Mkanganyiko wa majina ya wanawake

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Hakuna kipindi kigumu kama hiki ambacho majina halali ya wanawake huleta changamoto

Mwanamke hajaolewa hutumia majina ya wazazi wake wa kumzaa lakini anapoolewa hubadilisha hutumia jina la mume wake,je ndoa ikivunjika na akaolewa ataendelea kutumia majina ya mume wa kwanza?

Sasa hivi imeibuka tena kuwa hata kama mwanamke ameolewa aendelee na majina ya wazazi wake lakini wake wa viongozi wakubwa wanaendelea kutumia majina ya waume zao: lipi ni lipi sahihi?

Na kuna watoto wanaozaliwa,Single mothers wengine hukataa kuwapa majina ya wazazi wenzio kutokana na sababu wanazozijua na badala yake mtoto hutumia majina ya baba yake mama yake kwa lugha nyingine kama mwanamke anaitwa Jane Masanja na pia mtoto wa Jane anaitwa Mariam Masanja au Samwel Masanja...je ni sahihi wanawake kushare majina na watoto wao?

Nini kiondoe huu mkanganyiko?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mke wangu atumie jina la baba yake asijifanye ananijua zaidi ya baba yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…