Mkanganyiko wa maneno ktk matumizi ya lugha ya Kiswahili.

Mkanganyiko wa maneno ktk matumizi ya lugha ya Kiswahili.

Juma Bundala

Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
71
Reaction score
5
Ninataka kujua juu ya matumizi ya maneno haya WANGU,WAKE na ZAKE,ktk matumizi yafuatayo Mke,watoto, mme,changanyiko ni kama mke ni mmoja huwa ni mke WANGU lakini mtu akiwa na wake wawili huita WAKE ZANGU au WAKE ZAKE kama anasemewa,swali ni mtu akiwa na wanawake zaidi ya mmoja waitwe wanawake WAKE ama wanawake ZAKE? Mke mmoja sina shida
 
Huyu ni mke wangu, yule ni mke wake.
Hawa ni wake wangu, wale ni wake wake.
Pengine hapo ndipo waswahili waliona utata na kuamua kubadili neno 'wake' kuwa 'zake'.
 
Huyu ni mke wangu, yule ni mke wake. Hawa ni wake wangu, wale ni wake wake. Pengine hapo ndipo waswahili waliona utata na kuamua kubadili neno 'wake' kuwa 'zake'.
Nashukru kwa mchango wako,lakini ili maneno haya yatumike kwa usahihi tufanyeje?
 
Back
Top Bottom