Mkanganyo katika elimu ya kidato 1 - 6 Tanzania

Mkanganyo katika elimu ya kidato 1 - 6 Tanzania

Lovebird

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2012
Posts
6,383
Reaction score
9,337
Ndugu wana jamvi

Itakumbukwa tunatofautiana sana kielimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita

1. Mabadiliko ya mitaala imewafanya vijana wengi kuwa na upeo tofauti, viongozi walichanganya masomo kama jeografia/historia/uraia == likawa somo moja ....tukaendeleaaa mwishowe ikaonekana haifai WAKARUDISHA MFUMO WA ZAMANI

2. Michezo (umitashumta _ umiseta) mashuleniiii ILIFUTWA kabsaaaaa.....leo hii imerudishwaaaa

3. Sanaa ya jamii ... leo taa ikiungua chumbani/popote vijana hawamudu hata kuirudishia, mlango kitasa kimelegea hadi fundi aitweee, VIJANA wamebaki kuwa watazama tv na mitandao ya kijamiiii (nakubali ni mabadiliko)

4. Tumebadili namna ya kutoa matokeo ya kidato cha NNE na SITA, matumizi ya GPAaaaaaa........sikatai lakini tujiulize kwa baadae, unapopewa vyeti ukague kwa ajili ya matumizi ya maendelea itakuwejeee

****Kwa ufupi*****
1. Endapo yaliyokuwa yamefutwa yamerudisha na hili la GPA lifikiriwe upyaa (kwa walomaliza kabla ya mwaka 2014) warudishe vyeti NECTA wapewe vyeti vipya vinavyolandana na mfumo mpya
2. Tukumbuke pia baadhi wanapata misaada kusoma nje ya nchi Je mifumo inapokinzana kihivi wenzetu wanalitambua?
3. TUNAHITAJI kutathimini yote yafanyikayo kielimi

****MSINGI Mkubwa wa MAISHA ni ELIMUuuuuu...suprising WALIMU wa vyuo vikuu wanakimbilia SIASAAAA
 
Back
Top Bottom