Tunaendelea kukumbushana tuu kwamba hata hili la bandari siyo udini kama wazushi wanavyozusha.
Kipindi cha "Privatization" kilipopamba moto Hayati Rais Mstaafu Mkapa alitaka kubinafsisha shirika la ndege. Baraza la maaskofu TEC lilimuita na likamshauri kutokubinafsisha shirika hilo kwani ni kama "Mbawa" za nchi.
Vivyo hivyo kwenye hili la bandari wale mnaoshangaa TEC kutokukubaliana nalo basi hamuijui historia, bandari ni kama lango la nchi, ni mwendawazimu tuu ndiyo atakubali uwekezaji wenye mkataba aina ile, ambao unampa muwekezaji "Total Autonomy" muwekezaji ya kufanya chochote na nchi hairuhusiwi kuhoji chochote[emoji845][emoji845][emoji845]
Msikilize Padre Kitima hapa chini akitema madini kuhusiana na mambo ya uwekezaji.
Hapo ukimsikiliza anakuambia "Wamefanya Research" kabisa kwamba wawekezaji wazawa wasipopewa kipaumbele tutajenga taifa mfu ambalo muda wowote lotacollapse.
Ametolea mfano Ivory Coast ambapo waliwapa wawekezaji wa nje kila kitu bila wazawa kuwa na % kadhaa, mwisho wa siku nchi imekuwa unstable, mapinduzi kila siku.