Mkapa, Graca, Koffi Annan waingia mitini

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Maoni ya Annan yaliibua mjadala mkubwa kutoka kwa Wakenya wengine wakamchukia
Nairobi. Kundi muhimu ambalo lilisaidia kwa karibu kuunda Serikali ya Kenya ambalo lilikuwa likiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan halikuweza kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta.
Taarifa kutoka Kenya zilisema kwamba Kofi Annan ambaye aliongoza kuundwa kwa Serikali ya Muungano baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2007 hakuweza kuonekana katika sherehe hizo.
Pia waliokosekana ni wanachama wa kundi la Dk Annan ambao ni pamoja na Graca Machel na Benjamin Mkapa. Kundi hilo ndilo lilisaidia kuunda Serikali hiyo.

Lakini muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu, Annan alitaka uchaguzi nchini ufanyike kwa amani.
Mwaka jana , Annan aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alizua malumbano alipowahimiza Wakenya wasiwachague wanasiasa walioshtakiwa na Mahakama ya Kimataifa Kuhusu Uhalifu (ICC).
Ingawaje hakuwataja Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto, wanaokabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hiyo iliyopo The Hague, Uholanzi, Annan aliliambia shirika la BBC kuwa kuwachagua viongozi wa aina hiyo kutaathiri uhusiano wa Kenya na jamii ya kimataifa.
Maoni yake yaliibua majibu kutoka kwa wafuasi wa chama cha Rais Kenyatta cha The National Alliance (TNA) na wa United Republican Party (URP) cha Ruto.

CHANZO: Mkapa, Graca, Koffi Annan waingia mitini - Habari - mwananchi.co.tz
 
Lengo la hili kundi ilikuwa moja, na ilipobainika kuwa kenyatta amepata ushindi wa raundi one baada ya maamuzi ya mahakama ndipo, annan aliporodisha shukrani zake kwa mahakama kuu ya kenya bila kuzingatia wadau walioshiriki katika uchacguzi huo. Jambo hili huenda liliwauma sana kushindwa hata kuwapongeza wakenya kwa kupiga kura kwa amani.

Amani wakenya walioweka wakati wa uchaguzi unapongezwa kwa shughuli za ICC na media ya kimataifa, basi na kule sehemu zingine africa walipochokora na walete amani hiyo.

bure bilashi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…