Wewe makoye hata wewe uliwa rais huwezi kupitia kila kitu cha nchi hii unless uvunje safari na kila kitu ukae tu ofisini,mkapa tries his best lakini wasidizi wake nao walimuangusha na mjue mkapa sio mwanasheria hawezi kuelewa kirahis legal tems unless sahivi ajiriwe mwanasheria special na mwaminifu kwaajili ya kumtafsiria rais mikataba na kila kitu cha kisheria.wewe mwenyewe mkeo anaweza akawa analala na houseboy wako au mdogo wako na usijue sembuse mambo ya mikataba.simtetei mkapa ila tuongea vitu vya maana sometime ndio maana hata habari za kiwila siongelei kwasababu hiyo ile kweli alafanya makusudi.
Halafu mi nadhani baada ya kupiga kelele nyingi ohoo mkapa sasa tukubali yameshatokea tunafanya nini sasa????kama inawezekana kuvunja hito mikataba kwa gharama yeyote tufanye natujue vipi tunaingia mikataba yenye tija kwetu sio kila siku mara mkapa sofia simba sijui rostam mi naona ni kupoteza muda viongozi wetu ni kama sikio la kufa jamani.
Ikivilinge,
Kwenye management kuna kitu kinaitwa MBWA(Management By Walking Around). Kama Rais unapaswa kupitia kila sehemu siyo kukaa ofisini na kusubiri kuletewa rushwa,posho na hongo ili kutoa vibali vya kuuza nchi kama alivyofanya Rais wako Mkapa. Bado kuna maeneo Mkapa alikuwa akienda anapoona kuna ulaji(ufisadi)!
Tunaona Kikwete ana-practice hiyo MBWA. Mkapa alishindwa nini? Mbona alikwenda kule Bulyanhulu akapewa pande la Dhahabu?Mkapa hawezi kujitetea kwa lolote wala wale mnaomtetea haitasaidia. Mkapa ni FISADI tu mpaka kufa.
Sana sana wanaomtetea ni wale wakereketwa wa CCM au wale walionufaika na ufisadi kutoka kwake kwa namna moja au nyingine.
CCM yafaa tuibatize na kuipa jina la CHAMA CHA MAFISADI. Hili ni jina linalowafaa sana hawa jamaa kwa sasa.
Kwa taarifa yako Mkapa hana ubora wowote wa Urais katika karne hii hata Mo Ibrahim analijua hilo ndiyo maana alimtema kwenye kuteua Rais bora katika Afrika. Ninashangaa sana mtu anaposema eti Mkapa ni mojawapo ya Marais bora Afrika!! Kwa ubora upi hasa? Kama hata jumuia za Kimataifa zinashindwa kumtambua kama Rais Bora wewe unayosemaje kuwa ni Bora???
Kama kuna jumuia zingine za kimataifa wanaomuona Mkapa ni bora ni wale waliofaidika na utawala wake. Makampuni ambayo yamewekeza kwenye madini ili kuvuna Dhahabu na Almasi zetu ndo wanaomwona ni kiongozi bora, nje ya hapo Mkapa ni Rais BOMU kabisa katika kizazi hiki na karne hii.
The Way forward au kile tunachotakiwa kufanya ni kuipiga chini CHAMA CHA MAFISADI-CCM! Ili tuweze kuweka utawala wa chama kingine chenye mtazamo hasi na CCM. Haiwezekani CCM tangu TANU waendelee kuitawala nchi hii kana kwamba wana hati miliki ya Nchi hii. HAIWEZEKANI asilani.
Kumbukeni kuwa chama chochote kikishakaa madarakani kwa muda mrefu kinabweteka na kujisahau. CCM sasa hivi wamefulia wamebaki jina tu. Lazima waondoke Ikulu wapishe vyama vingine vyenye sera na mwelekeo tofauti ili kuikwamua nchi hii kutoka katika lindi la ufisadi na umaskini uliokthiri.
Lazima tujifunze toka kwa nchi zilizoendelea kama Uingereza, Marekani,Ufaransa,Ujeremani n.k.kuwa kila baada ya Chama kuongoza kwa muda fulani lazima chama kingine kichukue nafasi ili kuleta mabadiliko katika nyanja tofauti tofauti ambazo chama kilichotangulia kilishindwa kuleta mabadiliko na hasa mabadiliko ya kimaendeleo. Kosa tunalofanya Wa-tz ni kung'ang'ania kuchagua CCM kila mwaka. Chama ambacho kina sera na mipangi ileile ya miaka nenda rudi! Viongozi walewale,sera zilezile,sura zilezile,ufisadi uleule,ngojera ni zilezile hakuna jipya.
Sasa tunatakiwa Wa-tz tusema kuwa CCM basi imetosha. WE NEED CHANGE WHICH WE CAN BELIEVE IN kama alivyokuwa akitamka Rais wa Kwanza mweusi katika Taifa kubwa lenye nguvu duniani yaani USA mheshimiwa Barack Obama Onyango.
Kwa situation tuliyofikia Watanzania kwa sasa Change is inevitable and Change is a must. Nguvu ya sanduku la kura inatakiwa iamue na ituletee mabadiliko katika uchaguzi huu unaokuja wa 2010.