Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
David Musyoka ni Dereva wa Halmashauri huko Kenya, Kitui County.
Siku kaamka vizuri tu na kaenda kazini, akatumwa sehemu kikazi naye kama kwaida kawasha gari akaingia barabarani.
Mara akiwa barabarani anaendesha akaona watu wanashangaa ndege tai kashika nyoka.
Yule ndege tai akamwachia nyoka juu ya gari la Musyoka na akatokomea.
Huyo nyoka akaona dirisha la dereva liko wazi, hakukosea mara akingia ndani.
Musyoka kutaharuki, nyoka akamwuma mkononi na hakuachia akaendelea kuuma.
Musyoka akatoka ndani ya gari akipiga makelele, wale watu waliliona tukio wakasogelea na kumponda ponda yule nyoka na kumwua.
Cha ajabu sasa, wakati wale wasamaria wema wanamtafutia first aid Musyoka ikiwa pamoja na kusimamisha gari kumpeleka hospitali, yule ndege tai akatokea tena na kumchukua yule nyoka na kutokomea naye angani!
Sasa hapa tunahitaji PhD ya Mshana Jr kudadavua tukio.