The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 822
- 2,095
Kwa kawaida, Kambona alijua au alikuwa amearifiwa mapema kuhusu maasi ya Dar es Salaam katika vitengo vya usalama vya Tanganyika na maafisa wa Kiingereza ambao bado waliitumikia Serikali ya Tanganyika, lakini hakuchukua hatua yoyote kuikabili hali hiyo hadi pale ilipotokea. Mmoja wa maafisa hao ni Luteni Kanali Rowland Mans. Ilidaiwa kuwa, mara kwa mara, Kambona, akiwa Waziri wa Ulinzi, aliwatembelea maafisa wa ngazi za chini katika Kambi ya Colito, na mara nyingine, bila kuonana na viongozi wakubwa wa kambi hiyo.
Pia, kwa sababu zilizofichama lakini ambazo inawezekana ni njia ya kumsaidia Kassim Hanga, Kambona alitenga silaha na zana nyingine za vita zilizotoka Algeria na kuwasili Dar es Salaam, Jumatano ya tar. 3 Januari , mwaka 1964, na kupakuliwa chini ya ulinzi maalumu. Silaha hizo ziliwasili siku tisa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar na majuma mawili kabla ya maasi ya Dar es Salaam. Silaha hizi, baada ya maasi yaliyotokea Dar es Salaam, inadaiwa kuwa (yaani hakuna ushahidi bali nusu ukweli) zilichukuliwa na kutoswa baharini na Jeshi la Maji la Uingereza lililoombwa na Serikali ya Tanganyika Jumamosi ya tar. 25 Januari, mwaka 1964, kukomesha maasi ya jeshi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, silaha hizo, nyingi ya hizo, zilitumiwa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Kaskazini mwa Afrika. Zilitumiwa na Waingereza, Wajerumani, na Waitalino na zingekuwa vigumu kutumiwa katika miaka ya 1960, kwa kuwa hazikuwa na vipuri.
Kwa namna nyingine, inasemekana kwamba silaha hizo ziliagizwa na Serikali ya Tanganyika kwa ajili ya Chama cha Frelimo cha Msumbiji, ambapo silaha hizo zilipowasili jijini Dar es Salaam, pamoja na kwamba maafisa wakubwa wa Jeshi la Tanganyika walikuwa ni Waingereza, silaha hizo zilipakuliwa na wanajeshi Waafrika tu. Pia, inasemwa kwamba silaha hizo hazikuhifadhiwa kama ilivyopaswa, kwa hiyo zikawafanya Waingereza wagutuke. Walipozichunguza sana wakagundua kuwa zana nyingine zilitiwa alama ya msalaba mweusi, wakachukulia kwamba hizo zilizotiwa alama zilikusudiwa kupelekwa Zanzibar kumsaidia Kassim Hanga kulingana na tetesi walizokwisha zipata hapo awali. Lakini, silaha hizo hazikuwahi kufika Zanzibar. Hali hii nayo ilizua swali lingine. Je, zilikusudiwa kutumika wakati wa maasi yaliyotokea Dar es Salaam?
Kwa mujibu wa utafiti wa Ndugu Nestor Luanda katika kitabu cha Tanganyika Mutiny mara kwa mara, Kambona alienda katika Makao Makuu ya Jeshi mwishoni mwa 1963 na aliwaambia maafisa wa kijeshi wa Kiingereza kwamba alitaka wawe wameondoka nchini ifikapo mwishoni mwa 1964. Kambona alitaka maafisa wengi wa Kitanganyika wapewe vyeo haraka, jambo ambalo Waingereza walidai haliwezi kutendeka kwa ghafla kama alivyotaka. Kuanzia hapo, maafisa hao wakaanza kuwa na wasiwasi kuwa chochote kinaweza kutokea. Ingawa uhusiano wa maafisa wa kijeshi wa Uingereza na Waziri Kambona ulianza kupungua, huo si ushahidi wa kutosha kueleza kuwa Kambona alihusika kwa njia ya moja kwa moja au ya mzunguko.
Hata hivyo, usiku ule wa maasi, maafisa wengi wa Kiingereza walikamatwa na kutiwa ndani katika Kambi ya Colito ambako kwa wakati huo umeme tayari ulikwisha katwa. Kikosi kiasi cha wanajeshi ishiriki na watano (25), kikiongozwa na mwanajeshi machachari, Sajenti Francis Hingo Ilogi, mzaliwa wa Bukene, Tabora, waliondoka kambini hapo kwenda Ikulu kumfuata Rais, Mwl. Nyerere. Wakati huo huo, Mkuu wa Tawi Maalumu, Emilio Mzena, baada ya kuambiwa yaliyotokea na kwamba wanajeshi walio na silaha wameelekea Ikulu, aliwaarifu watu wake waliokuwa Ikulu na kuwaambia wamtoroshe Rais.
Mzena aliambiwa kuhusu maasi hayo majira ya saa 8:00 za usiku. Nusu saa baadaye, saa 8:30, baada ya kuamshwa na walinzi wao, Mwl. Nyerere, akiongozana na Makamu wake, Rashidi Kawawa, chini ya mlinzi wake mkuu bwana Peter DM Bwimbo waliondoka Ikulu kupitia mlango wa nyuma na kuvuka kwa pantone hadi Kigamboni. Walipishana na wanajeshi hao kwa sekunde chache tu, yaani ilikuwa ponyaponya. Baadaye, wanajeshi hao walipelekwa kwa Oscar Kambona, wakamchukua kwenda naye kambini kwao, Colito. Wakati huo, ghasia na uporaji wa mali za raia tayari ulikwisha tanda katika mitaa ya mji wa Dar es Salaam. Wakati hayo yakitokea, tayari walikwisha anza kupeana vyeo, huko huko kambini. Wengine walipokea vyeo hivyo lakini wengine hawakuharakisha kupokea. Kwa mfano, Ilogi ambaye alikuwa na cheo cha Sajini alijikuta katika cheo cha Luteni Kanali na wengine walimtaka mtu kama Kapteni Alex Nyirenda kuwa Brigedia.
Maasi hayo yalisababisha ghasia nyingi mitaani, hususan Mtaa wa Msimbazi, maeneo ya Kariakoo. Maeneo mengi ya katikati ya mji, risasi zilirindima pah pah pah! Mwarabu mmoja eneo la Magomeni, kwa kuona duka lake linavamiwa, alimpiga risasi mwanajeshi mmoja aliyejulikana kwa jina la Kassim. Koplo Nashon Mwita, ambaye alishuhudia mauaji hayo, alirudi kambini kujizatiti. Akiongozana na askari mwingine, Luteni Mwakipesile, pamoja na wanajeshi wengine, walifika Magomeni na kum’miminia risasi, Mwarabu huyo.
Kana kwamba haikutosha, waliiteketeza nyumba yake kwa moto. Katika nyumba hiyo, inasemekana, Mwarabu huyo aliteketea na familia yake ya watu kumi na watano (15).
Maasi hayo yalianza kusambaa haraka. Siku moja baadaye, Jumatatu ya tar. 20 Januari, yalifika hadi Kambi ya Jeshi ya Tabora ambako wanajeshi wengi, kama Mrisho Kapteni Sarakikya, Luteni David Msuguri na Luteni Abdallah Twalipo walipandishwa vyeo. Jumanne ya tar. 21 Januari, maasi hayo yakafika Nachingwea, kambi ambayo ndio kwanza tu ilikuwa imeanzishwa, ikiongozwa na Meja Temple Morris. Jumamosi ya tar. 25 Januari, mwaka 1964, baada ya kuona mambo yanakwenda halijojo, Mwl. Nyerere aliomba msaada kutoka Serikali ya Uingereza