UPDATE 19 MAY 2020
Mwendelezo kuhusiana na kazi ambayo mhusika aliletewa na Mr. T
Zaidi ni kuwa safari hiyo ilikuwa na ughafla wa aina fulani uliokuwa unaashiria KAMA mhusika alitakiwa aondoke pasipo watu wengi kujua. Akakumbuka pia mwaka 1999 aliwahi kukumbana na hali ya namna hiyo wakati akiwa anasaka ajira ya kudumu.
Kumbuka kuwa maelezo haya ameyaleta kwa ajili ya kugusia kidogo tu uhusiano uliopo mpaka sasa, kati yake na Mr. T, ambaye alimthibitisha kuwa tayari yeye ameshapokea malipo zaidi ya million 50 kama malimbikizo.
Msomaji inabidi akumbuke pia kuwa hapa mhusika yeye alikuwa tayari ameshasimama kudai maslahi yake miezi kadhaa nyuma, baada ya kuona kuwa mchakato huo unakuwa wa hatari kwake.
Hata hivyo, pamoja na taarifa hizi za Mr. T, mhusika:
- Yeye bado hajalipwa malimbikizo hayo mpaka leo
- Kwa hiyo inaonyesha KAMA wote Mr T pamoja na Mkuu wa Idara walikuwa na nia ya kum-trigger aanze tena kufuatilia maslahi hayo, na ndiyo maana hajaweza kulipwa mpaka leo
- Na kama ni kweli kwamba walikuwa na nia ya kumuanzisha ili aanzishe tena mchakato wa kudai masslahi hayo, basi obviously kulikuwa na set-up ya mitego mingine mipya kwenye mchakato wa kudai maslahi hayo
Hata hivyo, mhusika pamoja na kupata taarifa hizo nzuri kutoka kwa Mr T, bado hakuweza kuwa tempted kubadilisha msimamo wake, aliendelea na msimamo wa kuendelea kuusitisha kwa muda mchakato huo
KIKAO (CHA PILI) CHA DHARURA NA AMBACHO KILICHOITISHWA NA MR X
- Tofauti na kile cha mwanzo ambacho kilimhusisha Mr T, hiki cha pili kilikuwa ni rasmi
- Kilikuwa ni cha dharura, na kilifanyika mwezi wa pili mwishoni au wa tatau mwanzoni
- MR X alimfuata mhusika ofisini kwake na kumkaribisha mhusika kwenye kikao hicho kikiwa na agenda ya moja tu ya kumthibitishia kuwa atarekebishiwa maslahi na mshahara wake March 2020 na hatimaye malimbikizo ya mshahara huo mwezi unaofuata; maslahi ambayo amekuwa akiyadai kwa takribani miaka mitano (5) sasa
- Kikao hicho kilihudhuriwa na watu takribani 6 wenyeji pale ofisini, na mtu mwingine mmoja mgeni kutoka nje ya ofisi, na ambaye ni mstaafu wa pale, ila alikuwa akifanyia idara nyingine
- Kwa hiyo, Mr X alimfuata mhusika ofisini kwake siku hiyo na kumuomba ahudhurie kikao hicho cha dharura akimweleza kuwa yeye ndiye alikuwa ni mdau mkubwa wa kikao hicho
- Mhusika alikubali na alihudhuria kikao hicho na ambacho kiliweka wazi kuwa mwezi huo huo, ambao ulikuwa ni March 2020, angelipwa mshahara uliorekebishwa na kwamba malimbikizo ya mshahara huo uliorekebishwa, yangefuata mwezi unaofuata, yaani baada ya ule wa malipo ya mshahara mpya
- Mkuu wa Idara hakuwepo kwenye mkutano huo ila ilionyesha wazi kabisa kuwa waliokuwa waki-coordinate mkutano huo walikuwa na mandate yake, yaani alikuwa amewa-authorise kuendesha kikao hicho
- Hata hivyo hadi leo, hali haijatokea sawasawa na minutes za kikao hicho
Pamoja na kwamba hali haijatokea hivyo mpaka leo (May 2020) kwa maana kuwa hakuna malipo yoyote ambayo yameshafanywa kwa mhusika kulingana na minutes za kikao hicho, bado mhusika hana sababu yoyote ya kutilia shaka kilichojadiliwa kwenye kikao hicho
HATA HIVYO: Mhusika anaona KAMA Mr X alimpeleka mhusika kwenye kikao ambacho pengine
- HAKIKUWA SHAHIHI na wala taarifa zake hazikuwa sahihi, nia ikiwa ni kum-trigger mhusika aanze kupita pita tena kwenye ofisi ambazo huko mwanzo alikuwa ameamua kuacha kupitapita kwa sababu alikuwa tayari ameshaona hatari katika mchakato huo
- KILIKUWA SAHIHI isipokuwa taarifa zake kwamba malipo yake yangeweza kufanyika mwezi huo hazikuwa sahihi, nia yake ikiwa ni ile ile ya kum-trigger mhusika aanze kupita pita tena kwenye ofisi ambazo huko mwanzo alikuwa ameamua kuacha kwa sababu alikuwa tayari ameshaona kuna hatari katika pita pita hizo
- Alifanya hivyo baada ya trigger ya Mr. T (aliyedai kulipwa zaidi ya million 50) kuwa imeshindwa kufanya kazi
Hii inatkna na ukweli kwamba vikao vyote viwili vinaonekana kuwa na taarifa ambazo haziko sahihi sana, na hivyo kumfanya mhusika kuwa na notion kwamba wote Mr X na Mr T walikuwa na nia ya kum-trigger ili aanze tena kupita pita kwenye maofisi ya watu ambao tayari ameshayaogopa.
Zaidi ni kuwa mahusiano yaliyopo kati ya mhusika na watoa taarifa hizi njema, na kama alivyoyaainisha kwa kifupi sana hapo juu, hayako sawia sana kiasi cha kumfanya mhusika asiwe katika hali ya kiwango ambacho angeweza kuendelea kuwaamini tena, kama ambavyo anaweza kuwaamini binadamu wengine wa kawaida. Ni kwa sababu muda wote wako tricky na kwa ndani siyo watu ambao anaweza akasema kuwa ni marafiki kwake
Kwa hali hiyo basi, assuming sasa mhusika angepata shauku ya kutaka kujua ni nini kinaendelea kuhusiana na maslahi yake, halafu akaamua kuyafuatilia kwenye ofisi husika, na kwa bahati mbaya katika kupita pita kwenye maofisi ya watu, kukatokea chochote kile ambacho ni cha madhara kwake, picha ya haraka haraka ambayo ingejitokeza ni kuwa mhusika angekuwa responsible kwa madhara yale ambayo yangempata, kwa sababu lazima watu wangehoji, kama huyu mtu alikuwa ameamua kusitissha mchakato wa kufuatilia maslahi hayo, na akatangaza hivyo hadharani , je kilichomfanya auanzishe tena ni nini? Wengine wangeweza hata kufikia conclusion kuwa kwa vile alikuwa anadai maslahi, possibly ameshafrustrate na hivyo alikuwa katika mchakato wa kuwadhuru wengine, isipokuwa kwa bahati mbaya madhara yakamrudia yeye mwenyewe
MWANDISHI WENU ATARUDI KWA MATUKIO ZAIDI YASIYO YA KAWAIDA, YANAYOMHUSISHA MR X NA WASHIRIKA WAKE