Mkasa wa kuhuzunisha wa vijana watatu wa Chuo Kikuu

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
```Vijana watatu wa chuo kikuu hawakufanya mtihani kwa sababu hawakusoma na hawakujiandaa.

Wakaja na mpango, wajichafue na oil chafu kisha waende kumwona mwalimu wao wa chuo.

“Mwalimu tunaomba samahani hatukuja kwenye mtihani. Tulikuwa tumehudhuria harusi na wakati tunarudi gari letu lilipata tatizo na hivyo tukachafuka sana kama unavyo tuona”. Mwalimu wa chuo aliwaelewa na akawapa siku tatu wajiandae.

Baada ya siku tatu, walienda kwa Mwalimu wao wa chuo wakiwa wamejiandaa vizuri kwaajili ya mtihani maana walikuwa wamesoma.

Mwalimu wa chuo aliwaweka kwenye madarasa matatu tofauti na kuwapa maswali manne tu kwenye karatasi ya mtihani;

1. Nani alikuwa anaoa au kuolewa? (Alama 25)
2. Sherehe zilifanyika wapi? (Alama 25)
3. Ni wapi hasa gari lilipopata tatizo? (Alama 25)
4. Gari ilipata aina gani ya tatizo?(Alama 25).

Majibu ya kusahihishia: Majibu yenu lazima yafanane.

Hivi tunavyoongea bado wapo kwenye mtihani.```

*Somo: Ifahamu kweli nayo kweli itakuweka huru. [emoji2]*[emoji2][emoji23][emoji23][emoji23]
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Sema sisi ilitukuta tukiwaa darasa la sabaa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Sema sisi ilitukuta tukiwaa darasa la sabaa
Hahahaha
 
Hakuna rangi waliacha kuiona aiseeee! Dadeek!
 
[emoji23][emoji23][emoji23] nina uhakika simu zao ziliwasaidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…