Mkasa wa kweli: Nilifanywa boya kwa zaidi ya miaka kumi na mitatu akidai ana mtoto wangu

Duh mkuu ndiyo udanganywe kuwa kaenda Canada kusoma hata using'amue whasapp anatumia code number gani? Ama kweli urozi uko duniani.
 
Kaka kama hii hadithi ni ya kweli tunashukuru sana kwa kutushirikisha, ili tuweze kujifunza lolote juu ya maisha ya wanawake mahusiano na malezi ya mtoto na familia kwa ujumla. Makosa ulioyanya kwetu yanakuwa ni mafunzo na tahadhari pia.

Nimefurahi pia mlivyomalizana kwa amani na mume wa huyo mama, ingependeza wanaume tuwe hivi inapotokea tumegonganishwa na hawa wenzetu, wao wataendelea kubaki second tu hata wafanyeje na sisi tutaendelea kuwa first hata watufanyeje.
 
Kuna demu alishawahi kunichomekea ana mimba yangu nikasema poa tutalea

Hapo nilikutana nae Iringa yeye anaishi Arusha akanitumia mapicha ya vipimo nikasema hamna shida

Siku moja nikiwa Babati kikazi nikamfanyia shambulio la kushtukiza nikamwambia nipo Arusha tuonane akaleta janja janja

Kumbe alikuwa muongo hana mimba na hivyo vipimo alinitumia ni vya mimba ya dada yake walikuwa wamepanga wanipurure mapesa ya kulea mimba na malezi ya mtoto nikawazidi kete

Mchakato mzima mpaka nastukia walishanipurura kama laki 3 lakini walau niligundua mapema

Hawa viumbe wakikwambia ana mimba yako usikubali kindezi anaweza kuwa ana mimba kweli lakini mnahudumia watu kama saba hivi.

Naomba kuwasilisha ndugu wajumbe.
 
Na huu uzi uwe fundisho pia kwa wanaume wanaoendekeza michepuko
Mpigwe matukio zaidi na zaidi.
 
Ndio maana nikasema nitumie jamii forum kuwaonya wengine na kuacha kuzini na madhara nilioyapata Mimi kwa Sasa nimetulia na bi mkubwa wangu.
😂😂Ni vizuri lakini haiondoi maumivu umekosea sana mkeo, umetumia nguvu zake kuwekeza kwenye uzinzi, muda wake na ukampuuza kihisia, ushapigwa tukio ndo unaona thamani ya mke wako huu ni unafiki
 
Wanaume huwa mnadhani mna ujuzi wa kutupiga matukio na mnatuonaga wajinga ila siku mwanamke akiamua akupige tukio hadi shetani anakaa pembeni kuchukua notes.

Ndo mtuliege na wake zenu majumbani

Ukubwa dawa

Alafu aliekwambia kuna shule ya milioni mbili masaki nani?
 
Simlaumu huyo dada nakupa lawama wewe ndio boya.
 
Kuna Dem wakati naanza kazi nlipata.
Nilimpata kupitia Dem wa mshikaji wangu intake moja.
Nikawa natumia, bila malengo nae. Ikawa analeta habar za ndoa nakwepa.
Yule manzi sikumwelewa tabia zake. Nlihisi alikuwa mwepesi Sana kuachia kwa jamaa wengine.
Nlikuwa makini na matumiz ya ndom. Kuna siku nlijichanganya nikamla peku, ikawa msala.
Hakuchelewa akaleta habar nimempa mimba. Kwa kasi akataka nikae nae gheto.
Niliikubali ile mimba, na kumtunza mpaka ajifungue. Lakini sio kumuoa. Ndoa za mimba sizifagiliagi. Alikomaa na Mimi nikakomaa kwenye msimamo wangu.
Alikuja kupotea ghafula,sikujua alienda wapi.
Nilifatilia kwa ndugu zake, wakanambia aliolewA. "We siulimkataa, ulidhani hatapata mume. Nikawa mpole.
Siku moja tukaonana akiwa amejifungua.
Niliyogundua baada ya kuonana.
Mtoto hafanani na Mimi
Hakutaka tuongelee mtoto
Alikuwa na wasiwasi.
Niliishia kumsalimia, nikapita Kama simjui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…