Mkasa wa Majonzi: Je, ni mila zitakuwa zimesababisha huyu binti kujiua?

Mkasa wa Majonzi: Je, ni mila zitakuwa zimesababisha huyu binti kujiua?

Tsyamatsy

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2023
Posts
265
Reaction score
421
Jamii, mkasa huu ni wa kusikitisha Sana.

Jana majira ya saa 1 kasoro jioni kitongojini kulitolewa tangazo la bint mwenye umri Mimi nakisia ni Kama miaka 14 kuwa amepotea toka majira ya mchana alienda kutafuta kuni Hadi majira hayo ya jioni hajaonekana.

Ilipofika majira Kama saa 2 usiku huo, vilisikika vilio maporini kuashiria amepatikana lakini vilio viliashiria kupatikana kwake sio salama. Ukweli bint alipatikana lakini akiwa mahututi hajiwezi. Bint ni jamii ya Kimasai.

Tulikusanyika lakini jamii ya Kimasai walikuwa wengi na kujaribu kumpa huduma ya kwanza Kwa kumnywesha maziwa na kile ambacho waliamini kingeweza kumfanya atapike na kutoa sumu tumboni, inasemekana bint alikunywa sumu dawa za ng'ombe toka mchana Kwa lengo la Kujiua.

Kinyume na matarajio yake Ile sumu haikufanya Kazi Kwa haraka Hadi alipokwenda msituni kutafuta kuni ndipo alipoishiwa nguvu na kuangukia huko Hadi alipokutwa usiku huo, alipopelekwa hospital alifia huko Kwa mujibu wa jamaa zake.

Sababu za bint kujitoa uhai ni kwamba, bint huyo rika lake ni Kama miaka 14 Kwa mujibu wa Mila zao yeye alikuwa tayari ni mke wa mtu ila Kwa Mila zao alikuwa anaishi Kwa mama mkwe wake akipata uzoefu wa ndoa na mume wake alikuwa anafanya Kazi na Kuishi mbali.

Usiku wa kuamkia Jana mama mkwe hakuwepo nyumbani alisafiri, nyumbani bint alibaki na shemeji zake wawili, mmoja mdogo kwake na mwingine ni Kama rika lake, usiku huo alikuja jirani Yao Mmasai mwenzao akaingia ndani na kumtaka bint walale nae, bint hakukubali akaona atoke nje na kumwacha firauni ndani akamfuata shemeji yake wanaolingana na kumweleza kuhusu iyo kadhia ya kutakiwa kulala na huyo bedui yeye kakataa, na akamuomba shemeji walale nje ya nyumba amlinde adi asubui.

Kulipopambazuka bint hakuwa na Amani, aliumia moyo, aliamua kutafuta dawa za ng'ombe na kunywa hatimaye kupoteza uhai.

Hizi Mila za kuoza wasichana ambao umri ni mdogo na hajakomaa kiakili ni hatari!
 
Back
Top Bottom