Mkasa wa wakimbizi wa Sudan na Apeth (na mikasa mingine)

"Usiku mmoja unaweza ukabadili maisha yako yote."

NIGHT SHIFT
 
SEOBOK (2021)

[emoji95][emoji95][emoji91][emoji91]
 
Mzeebaba uwe unazielezeako kidogo tunapata mshawasha wa kuzidownload, kuna nyingine story unasema hii kweli kali,
Usijali.

Niambie unapenda movies za aina gani?
 
SEOBOK (2021)

[emoji95][emoji95][emoji91][emoji91]View attachment 1776224
SEOBOK (2021)

Tanzu: Mapigano (Action), tungo za sayansi (Sci-fi) na Usisimuzi (Thriller)

KISA: Ki-Hun ni 'ajenti' wa zamani wa usalama wa taifa ambaye analazimika kurejea kazini kwa shughuli fulani maalum.

Kwa njia za kisayansi, ametengenzwa mtu mwenye mfanano wa kila kitu na binadamu halisi. Ukimuona, pasi na kuambiwa, huwezi hisi kuwa huyu ni roboti.

Na mtu huyo ama tuseme kifaa hicho kina siri ya maisha ya milele (eternal life), na hapa ndipo tabu inapoanzia kwani baadhi ya makundi na watu wadhalimu wanataka kumtia mtu huyu mikononi kwa ajili ya shughuli zao.

Sasa agent Ki-Hun anapewa kazi ya kumsafirisha afike salama!

Kazi pevu.
 

Katika hizi nimeiona 'Knives Out'.
Picha zake za promotion hazivutii ila movie nzuri huwezi amini ni ya 2019.
 
Katika hizi nimeiona 'Knives Out'.
Picha zake za promotion hazivutii ila movie nzuri huwezi amini ni ya 2019.
One of the Best Mystery.

Vipi kuhus Murder on Orient Express?
 
Sijaicheki hii. Katika ulizotaja hapo nilizopitia ni knives out na escape Room.
Hii orient ikoje?
Brother, kama uliipenda Knives Out, fanya kila namna uitafute Murder on Orient Express. Inahusu mauaji yaliyotokea ndani ya treni ikiwa safarini.

Sasa kuhusu nani ni muuaji ndipo utata ulipo maana kila abiria ni mtuhumiwa mbele ya macho yako.

Bwana mmoja kama 'Blanc' katika Knives Out ndo anaingia mzigoni.

Huwezi taraji. Huwezi kisia muuaji.
 
THE BIKE THIEF (2021) [emoji91][emoji91]

TANZU: Action

MKASA: Very simple and straight. Bwana mmoja anaingia matatizoni baada ya pikipiki yake anayofanyia 'delivery' kuibiwa.

Shida ni kwamba, ana familia kubwa inayomtegemea, na pasipo pikipiki kazi hamna kwahiyo atashindwa kumudu kuleta chakula mezani.

Boss naye haelewi kitu!

Hapa ndo' mwamba anabakia bila 'option' yoyote isipokuwa kumtafuta mwizi wa pikipiki yake, kufa ama kupona!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…