Mkataba ambao wakili kaushuhudia na kusaini lakini upande mmoja haukuwepo una uhalali kisheria?

Mkataba ambao wakili kaushuhudia na kusaini lakini upande mmoja haukuwepo una uhalali kisheria?

Duniahadaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2017
Posts
336
Reaction score
677
Kuna jamaa yangu yamemfika. Habari kamili ni kuwa waliandikiana mkataba na kandarasi ili a supply material katika site iliyopo Rukwa. Huyo bosi mndarasi alikuwa Mbeya (anakoishi). Hivyo wali draft mkataba na kutumiana kwa email na kila mtu akaridhia vipengere. Mkandarasi ali saini huko Mbeya kisha aka- scan na akautuma kwa email, jamaa (supplier) aka u- print Rukwa na kisha kumpelekea mwanasheria (wakili) naye aka saini na kugonga muhuri kuwa ameshuhudia. Ukweli ni kuwa hapo ofisini alikuwa yeye tu na yule supplier.

Jamaa aka -suply material ( mawe, mchanga, kokoto). Kilichotokea ni kwamba mkandarasi aligoma kumlipa pesa ya yale material kwa kigezo kwamba hayakuwa na kiwango (ingawa yamejengewa). Supplier kaenda mahakamani na ule mkataba, yule mkandarasi kaamua kumruka kwamba hapakuwa na mkataba wowote kati yao na anasema anataka kuona mkataba original na wakili aliyeshuhudia kama anamfahamu.

Swali (1) Je, huo mkataba ni halali kisheria? (2) Je, mahakama itapokea huo mkataba kama kilelezo? (3) Je, wakili aliyedai kushuhudia wakati upande mmoja haukuwakilishwa, alikosea? (4) kama alikosea na ikathibitika, adhabu yake ni ipi?

WANASHERIA TUSAIDIENI.
 
Namba 3 hapo juu wakili alisaini kama shuhuda
 
Back
Top Bottom