Verrazanno
JF-Expert Member
- Sep 15, 2021
- 454
- 1,011
Associated Press
Djibouti walicheza ngoma bandarini siku ya kwanza.
Leo Djibouti wanalia machozi, DP World wamefukuzwa, Djibouti wanasema wameibiwa, wamelipa madola ya mafaini na magharama ya kesi za kimataifa. Hukumu ya siku za karibuni ilitoka mwezi May 2023 Washington DC.
Kesi mahakamani ni kwamba DPW, kwa sababu ya mtandao wake mpana majini na ardhini, walitumia vichochoro mbadala kupitisha bidhaa za wateja wa Djibouti (Ethiopia na Somalia) bila kuinufaisha Djibouti. Djibouti wakawafukuza, wakashtakiwa Uingereza. Wameshindwa kila kesi, kila rufaa. Wanalia machozi. Mzungu akisaini mkataba au akizindua biashara hachezi chezi ngoma kwa saab anajua yakienda kombo picha ya ngoma itatumika kumcheka. Turudi Tanganyika na jirani zake.
DP World na Rwanda.
Hivi tunavyoongea tayari kuna mahusiano ya kiuchukuzi kati ya Rwanda na DPW. Website ya DPW inasema wanai service Rwanda kwa kutumia barabara na bandari za Mombasa na D'Salaam. Kwa hiyo jamaa wana uwezo na upeo wa kutumia bandari yako kufanya biashara na wateja wako wa bandari bila hata kumiliki hiyo bandari yako. Wakimiliki inakuwaje?
DP World na DRC Congo
Mwaka wa juzi 2021, DPW walifunga MOU ya kuendeleza bandari ya Banana Port. Mwaka jana 2022 Dubai ikalalamika kwamba DRC imekuwa goigoi kuendeleza makubaliano yao ya Banana Port. Hii iko upande wa pili wa Afrika kule Atlantic, ambako DPW ikianza kazi kule huku Tanganyika hatuoni chochote kinachoendelea.
Kwa hiyo basi, DPW itakapokuwa ina run bandari za DSM, ya Banana, na Kigali (bandari kavu) watakuwa wanachakata mizigo kwa namna ambayo ina maximize profit kwao wao DPW. Watatumia computer algorithm hizo hizo zilizofanya tuwalete tuliposema "mifumo haisomani." Sasa itasomana kisawa-sawa. Nchi nne. Lakini itasomana kutokea Dubai, nyinyi hamtapewa muisome. Computer itachagua the most profitable route for DPW, sio TPA.
Mkataba unatubana sisi kujifunga na DPW lakini hauibani DPW kutofanya biashara na wateja wetu. DP World wanaenda kupoka biashara ya TPA na jirani zetu.
For Tanzania, it's the most horrendous contract in all history.