Mkataba ni kama unaleta magawanyiko katika jamii; tukiuacha kunatokea nini?

Mkataba ni kama unaleta magawanyiko katika jamii; tukiuacha kunatokea nini?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Huu mkataba umeleta mganyiko katika jamii mgawanyiko mkubwa sana. Hivi tukiuacha tunakosa nini? Mbona kama madhara yanayoweza kujitokeza ni mengi ikiwa tutang'angania mkataba huu? Baada ya mgawanyiko unaweza kujitokeza nani atawapatanisha

1. CCM na Chadema
2. Serikali na wananchi
3. Muislam na Mkristo
4. Mprotestanti na Mkatoliki?

Waraka wa TEC Mimi ninavyoona ni kwamba umekuja baada ya Bunge, Serikali, mahakama kutoa maoni yao. Sasa Waraka wa TEC maana yake ni kwamba Wananchi wamekataa mapendekezo ya CCM, mapendekezo ya Bunge, mapendekezo ya Serikali, mapendekezo ya mahakama mapendekezo ya Serikali, Bunge na mahakama vimekataliwa, tumeamua twende makanisani na misikitini, je, tunaamini tutapata suluhisho? TISS muko kazini kweli? TISS mmejiridhisha kuwa KKKT na Sabato ndiyo wengi kuliko Katoliki na makanisa mengine ya kiroho.

Hivi hatuwezi kutafuta suluhisho jengine kuliko ku-involve hizi Dini? Serious?
 
Tangu lini nchi ikaongozwa na madhehebu ya kidini?

Mfumo halali kikatiba ya dola imetoa go ahead kwenye mkataba shida iko wapi?
 
Sawa.lakini kabla ya huu mkataba Nchi ilikuwa hauendi? Unajua yaweza kuwa tajiri lakini ukakosa amani? Muulize Zelensky.Hana hamu kabisa
Tutakosa hela na mizigo kufika kwa wakati
 
dawa ya ccm ni TEC na si chadema.... TEC wanatoa waraka siku moja ccm wanateseka takribani siku ya tatu sasa nakuendeleaa..TEC mmenifurahisha sana
 
Ni kweli Taifa limegawanyika kidini lakini sio leo bali ni miaka mingi sana nyuma toka nyakati za uhuru.

Hali hii imeendelea mpaka leo na tuko na amani kwasababu kundi moja limeweza kuliwin kundi lingine kifikra, japo hili kundi superior limejisahau au kwa makusudi linaona kama mambo ni sawa tu na linaweza kufanya lolote.

Tunakoelekea lile kundi linaloonekana dhaifu linaweza kuchukua mkondo mbaya na kuifanya nchi isiwe salama tena na hapa wale mamafia wa dunia watashuka na kuendelea kujilia vyao kwa kujipimia.

USHAURI: WATANZANIA TUPENDANE NA KUIPENDA NCHI YETU WENYEWE NA HIZI DINI TUZICHUKULIE TU KAMA IMANI NA SIO SEHEMU YA KUWABAGUA NA KUWANYANYASA WATANZANIA WENZETU.
 
It is better to be divided by truth than to be united in error. It is better to speak the truth that hurts and then heals, than falsehood that comforts and then kills.

Adrian Rogers
 
Back
Top Bottom