Mkataba wa Azam TV ligi kuu

Mkataba wa Azam TV ligi kuu

Yombayomba

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2006
Posts
818
Reaction score
214
[h=3]MANJI AUNGURUMA KUHUSU MKATABA WA AZAM TV LIGI KUU, ASEMA YANGA...[/h]

IMEWEKWA JULAI 29, 2013 SAA 7:33 MCHANA
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
HIVI karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi yampitoBodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia.

Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:


Watata; Viongozi wa Yanga SC, kutoka kulia Balozi Ammy Mpungwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini, Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji, Waziri George Mkuchika, Mwenyekiti Baraza la Wadhamini, Francis Kifukwe, Mjumbe Baraza la Wadhamini na Clement Sanga, Makamu Mwenyekiti wa klabu .


1. BODI YA TPL
1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe .. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.

2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.

2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.

2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.

2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:

2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.

3. MIGOGORO YA MASLAHI
3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.

3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka matakwa maalum muhimu zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.

3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.

4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.


5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA
5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."

5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (sponsorship agreement) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.

Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.

Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.

Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.


(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
 
YANGA wakae na AZAM TV waongee ili wamalize hizo tofauti zao.

Yanga kama wakigmea mechi zao, itakuwaje kwa mechi ambayo watacheza na timu iliyokubali udhamini wa azam tv?, hyo ina mana azam tv atanufaika bado na uwepo wa yanga ktka ligi kwa kuptia timu zlizopo kwnye ligi zlizo kubali udhamini wao.
 
Mbona watu wengi,tulilitegemea hili kuwa litajitokeza,Na hapa tatizo kubwa ni maslahi ya kibiashara ya MANJI,hakuna kitu kingine,ameona anayetoa udhamini huo ni mfanya biashara mwenzake,na ki2 kingine hawa wakina manji,wanapoona kuwa mtu anakuja na mipango ya kusaidia timu zote ili ligi iwe na ushindani,na kuzifanya timu zianze kujitegemea,hawapendi wanataka kila siku waonekane Miungu watu.shame on u.
 
hivi arsenal wanaweza kukubali mechi zao zionyeshwe man utd tv?

Mkuu nazan jina la AZAM TV ndio limekuchanganya, ila hiyo ni tofaut na SIMBA TV au tv zingine za club kwa bongo, hilo ni jina kma zilivyo tv zngne ambazo zipo, kama itv,etc.
Na ndio mana azam tv yupo mbion kutoa king'amuzi chake hv karibuni, hvyo itakuwa tv station iliyo hai sio ya part time.
 
Mkuu nazan jina la AZAM TV ndio limekuchanganya, ila hiyo ni tofaut na SIMBA TV au tv zingine za club kwa bongo, hilo ni jina kma zilivyo tv zngne ambazo zipo, kama itv,etc.
Na ndio mana azam tv yupo mbion kutoa king'amuzi chake hv karibuni, hvyo itakuwa tv station iliyo hai sio ya part time.

ok...azam tv iko owned na nani??....azam fc iko owned na nani??sijui kwanini ila mimi naona sio sahihi azam tv kuonyesha ligi ambayo timu yao inacheza.....nxt watachukua full udhamini wa ligi kama vodacom mtasema sio timu ni kampuni ya unga ndio inadhamini.
 
TFF wamezoea kutubuluza sana,ndio maana tumepigwa na uganda nje ndani ndani njee.
Huwezi kutumia ubabe kuonyesha mechi bila makubaliano.
 
Lakini hamuoni timu nyingi zitanufaika? Maana vilabu vidogo vitaongezewa uwezo wa kushindana. Tatizo ni km mdau hapo juu alivyosema, mgongano wa kimaslahi wa Manji, ili aendelee kuabudiwa.
 
Lakini hamuoni timu nyingi zitanufaika? Maana vilabu vidogo vitaongezewa uwezo wa kushindana. Tatizo ni km mdau hapo juu alivyosema, mgongano wa kimaslahi wa Manji, ili aendelee kuabudiwa.

azam fc itanufaika zaidi kupitia faida za azam tv ambayo faida zake zitaenda AZAM PLC?!ambazo zitarudi kuwa invested azam fc
 
Nimeisikia leo kwenye clouds fm katika kipindi cha jahzi kuwa bwana Manji alikuwa ni mmoja ya wagombea uenyekiti wa TPL board.

Lakini pia mwenyekiti wa mpito wa TPL board ni mfanyakazi wa Azam(cheo nimesahau),so hapo lazima kutakuwepo mgongano wa kimaslahi.
 
Mkuu nazan jina la AZAM TV ndio limekuchanganya, ila hiyo ni tofaut na SIMBA TV au tv zingine za club kwa bongo, hilo ni jina kma zilivyo tv zngne ambazo zipo, kama itv,etc.
Na ndio mana azam tv yupo mbion kutoa king'amuzi chake hv karibuni, hvyo itakuwa tv station iliyo hai sio ya part time.

Swala la msingi zaidi ni: iko wapi hiyo Azam Tv? Inakuwaje kwa kituo ambacho hata hakijaanza kazi au angalau kusajiliwa rasmi, kanze kufanya biashara tena isiyo na ushindani wa kisheria, au ni kwa ajili ya iina la anayekimiliki?
 
Tatizo kubwa hapa ni je tendering process ilifanyika? Kulikuwa na tangazo la kuzitaka tv icluding dstv kuleta quotation ili washindane? Kama jibu ni hapana, hao azam tv wamepewaje hiyo nafasi? Ni kigezo gani kimetumika?

Tibaa
 
Tatizo kubwa hapa ni je tendering process ilifanyika? Kulikuwa na tangazo la kuzitaka tv icluding dstv kuleta quotation ili washindane? Kama jibu ni hapana, hao azam tv wamepewaje hiyo nafasi? Ni kigezo gani kimetumika?

Tibaa

hamna tendering wala nini...juu kwa juu azam tv kapewa tender!
 
Yanga wanampango wakulifanya Taifa lisisonge mbele kimichezo. Ukiangalia kwajicho la ziada utagundua jinsigani Yanga walivyokua na wivu, hawataki mawazo mazuri yatoke kwa wenzao
 
Kweli na sawa na Man U kuonyesha EPL

AZAM TV sio TV ya klabu msipotoshe watu, ni business nyingine tu ya Bakhressa na wote mnafahamu biashara nyingi za Bakhressa zinatumia jina gani. What if Azam Fc isingekuwepo? Au Tv ingeitwa jina lingine, say PLANET TV? Yanga bado wangegoma sababu inauhusiano na Bakhressa mwenye Azam Fc? Hizi Simba na Yanga ni WACHAWI wa maendeleo ya soka yetu, wanajifanya wanajua huku klabu zao zinaendeshwa kama mwaka 1920!
 
Back
Top Bottom