Mpaka sasa ukiusoma mchezo unagundua suala la DP World ni la Chongolo na baadhi ya watu wake na sio dili la CCM kwa ujumla wake, mfano mdogo ni ziara ya Kinana tangu ameanza mikutano Rufiji, akaenda Kondoa na sasa yuko Manyara sijamsikia akipigia debe suala la mkataba wa bandari.
Ndani ya CCM ajenda hii ni ya Chongolo na watu wake wachache kama kweli ni jambo la Chama kwanini Kinana hazungumzi chochote kuhusu DP? Lakini hata Mwenyekiti mwenyewe wa CCM Samia ni wapi amewahi kutamka neno la kupigia debe DP? ukiona hivyo ujue hili dubwasha ni la watu wachache.
Soma hotuba ya Serikali ya Mwaka 2023/2024 kama utaona hata mstari mmoja unaozungumzia DP. ukimaliza hapo Msikilize Mstaafu Kikwete ameongea na vyombo vya habari siku za karibuni kama umemsikia amezungumza neno DP.
Ukifanya uchambuzi kwa kina utakubaliana nami kwamba Ishu ya DP ni ya watu wachache ila inataka kugeuzwa na kulazimishwa kwamba ni jambo la CCM. Wakati wana CCM wenyewe huku chini hawataki mkataba wa DP ila wanahitaji wawekezaji wa kuboresha na kuongeza mapato ya nchi.