Mkataba wa DP World unaweza kutufikisha kusikotakiwa

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Hatuwezi kwenda Makanisani au Misikitini kupambana na shetani asiyeonekana badala ya kupambana na shetani anayeonekana kwanza(DP World)

Nitoe wito kwa wanaohusika na mkataba huu wa DP World kwamba wanatakiwa kujibu hoja za msingi kutoka kwa Watanzania na siyo tu kujificha kwenye udini, ujinsi na Uzanzibar. Hoja hizo ni kama vile:-

1. Kama mkataba huu una nia njema, kwa nini haujahusisha Bandari za Zanzibar?

2. Kwa nini mkataba huu unavunja Katiba yetu ya Nchi?

3. Kwa nini mkataba huu unavunja hata sheria za kimataifa?

4. Je, ni kweli kwamba Watanzania tumeshindwa kabisa kuendesha Bandari zetu?

Nawasilisha.
 
Mwenyezi MUNGU sikiliza kilio cha Watanganyika na utende miujiza katikati yetu.
 
Reactions: YSK
Kwanini sa100 anaamua kuuza nchi ya Tanganyika kwa waarabu?
 
Ngoja tuone bndera ya waarabu ikipee pale bandarini
 
Nchi ngapi zinaitegemea bandari ya Zanzibar ?
Yaani umlete DPW aje aendeshe bandari inayoingiza meli 3 kwa mwaka ? Huko sindio kujitukana ?
Unaujua msemo wa "Jino moja mswaki wa nini" maanake ?
 
Mungu ana njia nyingi, si ukute ni mpango wa Mungu Tanganyika iibuke tena.
 
Mungu ana njia nyingi, si ukute ni mpango wa Mungu Tanganyika iibuke tena.
Mungu huwatia watu upofu pale anapotaka kufanya lake! Baada ya hapa hili saga litaibua msiyoyategemea.
 
Tumeshindwa kuendesha bandari yetu ndiyo , tunachojua Ni kuiibia serikali tu.
 
Nchi ngapi zinaitegemea bandari ya Zanzibar ?
Yaani umlete DPW aje aendeshe bandari inayoingiza meli 3 kwa mwaka ? Huko sindio kujitukana ?
Unaujua msemo wa "Jino moja mswaki wa nini" maanake ?
Unataka kusema hizo bandari za kwenye maziwa, ambazo zimeingizwa kwenye mkataba, zina meli nyingi kuliko bandari ya Zanzibar?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…