Mkataba wa Songas na TANESCO bora uvunjwe, hauna maslahi kwa Taifa!

Mkataba wa Songas na TANESCO bora uvunjwe, hauna maslahi kwa Taifa!

Macos

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2008
Posts
1,979
Reaction score
1,416
Mradi wa gesi ya Songo-songo unajulikana zaidi kama “Songas” - ambao unamilikiwa na kuendeshwa na kampuni ijulikanayo kama Pan African ni wa kijinga na hauna maslahi yoyote kwa mtanzania kwanini mradi huu ni wizi mtumpu!
  • Kwanza Tanzania haina mamlaka yoyote ya kibiashara katika mrado huo.
  • Eti Pan African wao tu ndio watazalisha gesi hiyo kuisafirisha kutoka Songo-songo hadi Dar es salaam kwa ajili ya kuzalisha umeme katika mitambo ya gesi ya kampuni yao nyingine SANGAS (hapa ni ujanja ujanja tu ili ionekene wanaozalisha na kusafirisha na kuzalisha umeme ni kampuni tofauti)
  • Songas wao 'wananunua' gesi kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO
  • TANESCO hawaruhisiwi kununua na kuendesha mitambo ya umeme na kutumia gesi hiyo ya Songo songo.
  • Songas wanapaswa kulipwa kitu kinaitwa ‘capacity charges’ na TANESCO eti kama Songas hawazalishi umeme na hizi ni kwa mabilioni kila mwezi
  • Kama TANESCO wanalipa capacity charges...... bili ya kutofanya kazi kwa Songas shs 3,000,000,000/= kwa mwezi basi kwa miaka zaidi ya 8 waliyoanza Songas kama utachukua wastani wa miezi 30. TANESCO hawakuhitaji umeme wa Songas, hawa jamaa wameshajichukulia zaidi ya 90 billions..!! na katika hiyo miezi mingine TANESCO wananunua umeme kutoka kwa Songas kwa bei kubwa
  • Hawa songas walijenga pipeline ya kusafirisha gesi ndogo wakati wanajua wazi matumizi ya gesi yataongezeka ila walifanya makusudi ili wafanye tena mradi wa upanuzi hivyo wamepata kisingizio cha kukopa na deni; hii itaonndoa nafasi yoyote ya serikali kuingia hapo na kufanya uzalishaji
  • Lakini kwanini serikali wakubali kupanua pipeline hii? Kuna maslahi gani?
  • Tunachohitaji kutoka na gesi ya Songo songo ni kuzalisha umeme basi... hatutaki gesi hiyo kutumiwa kwa kitu kingine. Sasa, ni wazo la mwanzo la kuzalisha umeme huko huko Songo songo ndio sahihi na lina maslahi.
  • Wakati ule kuna watu walipiga kelele kwamba ni bora hayo majenereta yapelekwe Songo songo na serikali igharamie kujenga nyaya hadi kwenye gridi ya Taifa.
  • Kama gesi ile ipo ya kutosha na serikali haijatapeliwa basi tatizo la umeme haliwezi kuendelea kwani kila mwaka tukiweka mkakati wa kupeleka generator moja huko Songosongo basi hata mvua isiponyesha karne nzima umeme utapatikana.
  • Kujenga na kuzalisha umeme kule Songo songo ni rahisi zaidi na investment yake ni mara moja.....yaani kuunganishwa na gridi ya taifa; lakini pipeline gharama yake ni kubwa ,, kusukuma gesi , maintenance yake ni gharama na sasa kama tulivyoona pipe ni ndogo inabidi iongezewe
  • Tunajua hawa wazungu waloshikilia mradi huu hawawezi kukubali kuitumia gesi yetu kujitosheleza na umeme lakini ni vyema ikataifishwa hawa jamaa wakalipwa fidia, tukazalisha hii gesi wenyewe kwa kuanzisha kampuni ya taifa ya gesi na wao watawauzia TANESCO kwa bei ya chini ya kibiashara.
  • Lakini maamuzi haya yanataka mwanaume wa kweli
  • Ni aibu kubwa kwamba nchi hii ina gesi lakini hatuwezi kuzalisha umeme na nchi ipo kwenye giza...aibu kubwa; lakini cha kushangaza hakuna hata mbunge ambaye analaumu kwamba mradi wa Songas tumehujumiwa...
  • Watanzania tunaonekana wa ajabu kweli kwenda kuomba omba wakati tuna gesi kuzalisha umeme.
  • Let’s go to China au Malaysia au India kama ni teknolijia inatushinda...
  • Ukweli tunahitaji mapinduzi makubwa ya akili ili tufike....kwa kweli hatuna sababu ya kuwa gizani..
  • Wabunge taifisheni Songo-songo, ni mradi unaoifilisi TANESCO.
 
Tunahitaji mapinduzi ya serikali, kwa kura au kwa shari. Nitaambiwa mchochezi au muhaini. Liwalo na liwe.
 
Back
Top Bottom