Mkataba wa TFF na TBC kila mwezi timu itakayoshiriki ligi kuu itapata Tsh.182,291?

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
Nashangazwa tu na kiasi hicho maana mkataba hapo wazi kama ule wa Azam.

Kwa miaka jumla ya thamani ya mkataba ni Bill 3.5 ukigawanya kwa miaka kumi ni Mill 350, hii ni kila mwaka.

Million 350 ukigawa kwa miezi 12 ni sawa na Million 2,916,666,hii ni pesa ya kila mwezi.

Million 2 na laki 9 ukigawa kwa 16 idadi ya timu zinazoshiriki liguu ambazo zitakuwa msimu ujao ni Tsh.182,291 kwa kila timu kwa kila mwezi ndani ya miaka 10?

Je, huu ndio tafsiri ya mkataba husika?

Faida za TBC kwenye mkataba huu.

Itaongeza wasikilizaji na sponsors kwenye utangazaji wao matangazo ya mpira mf.Kampuni ya Colgate ikitoa wakidhamini kila kwa laki 2 tu ili bidhaa yao itangazwe TBC watapata pesa yakuwapa TFF na chenji itabaki iyo kwa mechi 1.

TBC sasa ndio wanayo haki ya kuwauzia mashirika ya redio mengine yakitaka kutangaza mpira je watauza bei wanayoitaka na TFF hawana cha kufanya.
 
Nashangazwa tu na kiasi hicho maana mkataba hapo wazi kama ule wa Azam
Kwa miaka jumla ya thamani ya mkataba ni Bill 3.5 ukigawanya kwa miaka kumi ni Mill 350,hii ni kila mwaka...
Siyo kweli hapo hesabu milioni 350 ukigawa kwa miezi 12 unapata 29.166666666666666 milioni,

Hapo ukigawa kwa timu 16,kila timu itapata 1.8229166666666666 Milioni mkuu.

Kila timu itapata 1.8 milioni (milioni moja na laki nane ) kila mwezi


[emoji1][emoji1][emoji1][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] KARIA NI KIBOKO
 
Siyo kweli hapo hesabu milioni 350 ukigawa kwa miezi 12 unapata 29.166666666666666 milioni,

Hapo ukigawa kwa timu 16,kila timu itapata 1.8229166666666666 Milioni mkuu...
Kwa timu ina msaada kiasi chake kama kweli mgao utakuwa kama ulivyo assume.

Kwanza, hii deal haijawahi kuwepo kabla. Alichokosea TFF ni kuingia deal la miaka mingi kiasi hicho.

Pili, timu zinacheza ligi miezi takribani 6 lakini malipo ni miezi 12. So kuna malipo extra hapo bila kucheza mchezo wowote.
 
Kutoka matangazo kurushwa kiholela mpaka 291666 kwa mwezi sio mbaya. Sema mtanzania bora akose kuliko apate kidogo.

Mdogo wangu fulsa ndogo ndo inaanzisha safari yakuelekea fursa kubwa . Waza 1 then 2 ndo ufikirie 5,6,7,8,9,10... ko mbeleni tutapga pesa2.
, Mfn kwa miaka zaid ya 10 nyuma unajua ligi kuu soka Tz ilikuwa sh ngap na sasa tunaenda kupata sh ngap. Msiwe na haraka yakufika vijana wakat kuna vituo bado hat hatujavipita
 
Siyo kweli hapo hesabu milioni 350 ukigawa kwa miezi 12 unapata 29.166666666666666 milioni,

Hapo ukigawa kwa timu 16,kila timu itapata 1.8229166666666666 Milioni mkuu...
Unamiaka mingapi hujasikiliza mpira kwenye redio?
 
ni kweli mpira ulitngazwa bure lakini hizi redio zinapata pesa kupitia matangazo ya mpira kutoka kwa wadhamini hivyo lazima klabu zifaidike
Kwahiyo wewe unaumia wenye redio kupata faida au unamaanisha nini?
Mwaka jana tu hapo mpira ulikuwa ukirushwa bure kabisaa leo watu wamesign mkataba tayarii haraka haraka unakuja kusema sio wa faida na huku unajua hata hao wasikilizaji mpira kwenye redio wamepungua azam wamefika kila kona watu wanakuwa live sasa hao redio watoe mabilion kwa faida gani uliyo itathmin
 
Hizi Channel za serikali zinazingua sana, nakumbuka kama sio 2005,2006,2007 au 2008 super sports ilitangaza kulipa Rand 1M kwa msimu Kwa kila Club itayoshiriki ligi kuu ya South Africa ili waoneshe mechi zao,Channel ya serikali SABC1 wakalivuruga deal kwa kuwa hawakutakiwa kuonesha mechi yoyote. Wakachukua wao hili deal na kuzilipa Club hela kiduchu tu Kwa kuwa wao ni serikali.
Miaka kumi ni mingi mno!
Nalog off
 
kabla ya kuandika soma uelewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…