Mkataba wa TICTS haukuhitaji IGA, kwanini wa DPW uhitaji IGA?

Mkataba wa TICTS haukuhitaji IGA, kwanini wa DPW uhitaji IGA?

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
9,327
Reaction score
5,206
Kume kuwa na utetezi WA Wanaotetea nkataba WA DPW kuwa ukodishaji WA Bandari sio WA mara ya Kwanza , Kwa kutolea mfano WA Mkataba WA TICTS ambayo ilikuwa na muungano na Hutchinson ya Singapore , bula kuweka utofauti WA mikataba hii.

Mosi nkataba WA TICTS haukuwa na IGA lakini huu Una WA DPw Una IGA. Pili nkataba WA TICTS ilikuwa na ukomo Kwanza WA miaka 10 na baadae kuongezewa miaka 15. Ndio maana kelele za kuuzwa hazikuwepo.

Tatu kulikuwepo na nkataba kama WA IPTL ambao ilikuwa na kifungu cha kuwalipa USD 100m ikiwa tutavunja mkataba kabla ya kuisha miaka 10 , lakini nkataba huo unalitesa taifa zaidi ya miaka kumi sasa. Na hela zina chotwa kulipia capacity charge wazalishe umeme au wasizalishe na mengineyo, licha ya maneno mazuri tuliyopewa mikataba hiyo ilivyoingiwa.

Ndio maana Leo hii watu wanapiga kelele juu ya ukomo WA Mkataba huu, na jinsi ya kutoka kwenye ndoa hii ikiwa kuna vitu kwenda tofauti na matarajio yetu.

Sasa haya maneno haifai kujibiwa kisiasa Kwani haya masala sio la kisiasa na sio la kiuchumi Tu, Bali Lina mambo ya kisheria ambapo ndipo mgogoro mkuu ulipo na madhara take Kwa nchi yapo huko.
Hivyo hoja za kisiasa na za kiuchumi zisitumiwe kulaghai Taifa.

Nne kuna mkataba WA Loliondo ambao nao tuliambiwa ni miaka kumi lakini Hadi Leo bado Ortelo yupo na ndio maana watu wana ogopa hili suala la Maisha au milele. Na hatujui huo ukodishaji WA Loliondo fedha zake zinakwenda wapi na Taifa linapata faida katika nkataba huo. Na CAG report zake haziongelei suala hili kana kwamba Loliondo sio sehemu ya TZ.
 
Suala la Bandari Tumuombe saaana Mungu,, Hili suala Watu wanalipeleka kishabiki Kama Simba Na yanga..Tuache mkataba ujiteteee Siyo Watu watetee
 
Mambo ya ajabu kabisa....,

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Back
Top Bottom