Mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uwekwe wazi wananchi tuusome kuepusha upotoshaji unaoweza kufanyika

Mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo uwekwe wazi wananchi tuusome kuepusha upotoshaji unaoweza kufanyika

Joined
Jul 15, 2018
Posts
61
Reaction score
127
Habari ya leo wakuu,

Imani yangu nyote ni wazima, kwa wasio wazima InshaAllah Allah awafanyie wepesi.

Moja kwa moja kwenye hoja.

Naomba mkataba na project proposal ya ujenzi wa bandari ya kisasa ya Bagamoyo uwekwe wazi ili Watanzania wenye uwezo wausome, uchambuliwe pro and cons zake zote, ili kila mmoja anaetaka kupotosha, kukosoa, au kushauri afanye hivyo akiwa well informed.
 
Nchi hii bwana,kwanini tamaa ya miradi ya aina moja wakati midogo hatujaimaliza na kuisimamia.

Wakati wa mradi wa gesi mtwara tuliambiwa mtwara itakuwa Dubai.gesi yenyewe haijawafikia wananchi walio wengi.
 
Ni mkataba upi ambao ulishawahi kuwekwa wazi? Hiyo ya mindege, bwawa la umeme, ya gesi, madini? Leo huu wa Bagamoyo ndio uwafanye muuone una umuhimu wa kipekee? Watu wakipigania katiba mpya ili hayo mambo yasiwe ni kwa hiari bali ni lazima, mnawaona wanatumiwa na mabeberu!!acheni tu , time will tell
 
Nchi hii bwana,kwanini tamaa ya miradi ya aina moja wakati midogo hatujaimaliza na kuisimamia.

Wakati wa mradi wa gesi mtwara tuliambiwa mtwara itakuwa Dubai.gesi yenyewe haijawafikia wananchi walio wengi.
Ccm haijawahi kuwa sehemu salama
 
Write your reply...ni mkataba gani umeshawahi kuwekwa hadharani?
Mkataba hautakiwi kuwa wazi ila masharti ya wachina yenye utata yawekwe wazi kwanza ili tujadili then wahusika waone yapi ya kurekebisha kisha wafunge mkataba huo na kazi iendelee
 
Mkataba ukiwekwa wazi mkiona vile vipengele mliovyoaminishwa havipo mtasema sio huo, mfano mzuri ni ile ripoti ya CAG mlivyoona yule Karume kenge amepigwa nyundo za kichwa na miradi yake ya upigaji mkaanza kulalamika eti ile ripoti imechakachuliwa ili kuuwa "legacy" ya Karume kenge.
Hebu tafuta kuweka mambo sawa au usahihi, ni Karume Kenge au Kalume Kenge?
 
haiwezi kuwekwa wazi for security and safety reason kama taifa
labda wakwambie mradi utaanz lini utaisha lini nani anajenga
 
Back
Top Bottom