Mkataba wa ujenzi wa uwanja wa ndege Serengeti wasainiwa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkataba wa Ujenzi wa Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege Wilayani Serengeti umesainiwa Februari 27,2025 Jijini Dar Es Salaam

Utekelekezaji wa Mradi huo utasimamiwa Mhandisi Mshauri na Kampuni Binafsi ya 7-Engineering kwa kushirikana na Intairplan GMBH na Project Plus (T) LTD, kwa gharama za Sh 1.3 Bilioni ,muda wa utekelezaji ni miezi sita.

Utiaaji saini huo umeshuhudiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Dk Maulid Madeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Uwanja huo Dk Rhimo Nyansaho.

Kujengwa kwa uwanja huo kutasaidia kupunguza idadi za ndege zinazotua ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kusaidia kufungua fursa kwa wilaya na Mkoa wa Mara kwa Ujumla.
 
Twiga na pembe za ndovu Sasa zitaibiwa kwenye hifadhi ya Serengeti bila bugudha yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…