Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mkataba huu ulitiwa sahihi miaka mitano baada ya kifo cha Archduke Franz Fernand aliyekua mrithi wa Ufalme wa Hungary, Bosnia na Austria, hii ilikua falme moja kabla ya mgawanyiko.
Sababu ya mauwaji ilikua vuguvugu la wanafunzi wa Bosnia waliotaka Bosnia iwe huru kutoka katika utawala wa kifashist wa Ufalme wa Hungry-Austria. Kifo hiki ndicho kiliamsha mapigano na matokeo ya WWI.
Baada ya machafuko kutokea Austria Hungary, Ujerumani ilitangaza vita na Urusi lakini ilivamia Ufaransa na Ubeligiji. Baada ya hapa Uingereza ilitangaza vita na Ujerumani.
Katika mkataba wa Versaille, Ujerumani iloamriwa ilipe fidia ya vita na kuachia Makoloni yake yote.