Mkataba wenye utata kati ya Bernard Morrison na Simba umebadiliahwa rasmi kwenye mfumo wa usajili was TMS

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
KIDAO aagiza, Mkataba wa Morrison na Simba wabadilishwa rasmi TMS

Mkataba wenye utata kati ya Bernard Morrison na Simba umebadiliahwa rasmi kwenye mfumo wa usajili was TMS, baada ya Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred KIDAO kuwaamrisha maofisa wake kufanya hivyo usiku wa manane kuamkia leo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya TFF kitengo cha Usajili zinasema kuwa KIDAO alimuagiza mmoja wa maofisa wake wanaosimamia TMS, kufanya hiyo usiku na tayari zoezi limekamilika.

TFF ilikuwa ikisubiri kwa hamu dirisha la usajili kufunguliwa ili wabadili Mkataba wenye mapungu uliokuwepo na waweke mpya, ili kuzima malalamiko yaliyoibuliwa na Yanga Oktoba Mosi mwaka huu.

Tangu Yanga ilipoibua malalamiko hayo ya kukiukwa kwa taratibu za Usajili, TFF haikujibu chochote, huku Vigogo wa TFF wakikutana na wale wa Simba kwa siri kupanga namna ya kulizima sakata hilo na ndipo Rais wa TFF Wallece KARIA na Katibu wake KIDAO walipoagiza hoja za Yanga zisijibiwe huku wakiagiza wafanyakazi wa TFF kwenye mfumo wa Usajili kuhakikiaha wanabadili mkataba huo mara tu dirisha litakapofunguliwa.

Mara tu baada ya dirisha kufunguliwa saa sita Usiku, KIDAO aliwakurupusha Maofisa wake, kufanya suala hilo na tayari wamebadilisha Mkataba huo hivyo kujinuaufu na aibu kubwa ilivyokuwa ikiwakabili.

Baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko rasmi Oktoba Mosi, KIDAO alikataa Sekretarieti ya TFF kupelekwa suala hilo kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, na badala yake akafungua kesi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela kwenye Kamati ya Maadili.

KIDAO na KARIA wamekuwa mawakala wakubwa wa agenda chafu za Simba kwenye soka la Tanzania huku wakiendesha Shirikisho watakavyo wao bila kujali taratibu na kila anayeonekana kuwahoji wamekuwa wakimtafutia utaratibu wa kumfungia.

Mkataba wenye utata kati ya Bernard Morrison na Simba umebadiliahwa rasmi kwenye mfumo wa usajili was TMS, baada ya Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred KIDAO kuwaamrisha maofisa wake kufanya hivyo usiku wa manane kuamkia leo.

TFF ilikuwa ikisubiri kwa hamu dirisha la usajili kufunguliwa ili wabadili Mkataba wenye mapungu uliokuwepo na waweke mpya, ili kuzima malalamiko yaliyoibuliwa na Yanga Oktoba Mosi mwaka huu.

Tangu Yanga ilipoibua malalamiko hayo ya kukiukwa kwa taratibu za Usajili, TFF haikujibu chochote, huku Vigogo wa TFF wakikutana na wale wa Simba kwa siri kupanga namna ya kulizima sakata hilo na ndipo Rais wa TFF Wallece KARIA na Katibu wake KIDAO walipoagiza hoja za Yanga zisijibiwe huku wakiagiza wafanyakazi wa TFF kwenye mfumo wa Usajili kuhakikiaha wanabadili mkataba huo mara tu dirisha litakapofunguliwa.

Mara tu baada ya dirisha kufunguliwa saa sita Usiku, KIDAO aliwakurupusha Maofisa wake, kufanya suala hilo na tayari wamebadilisha Mkataba huo hivyo kujinuaufu na aibu kubwa ilivyokuwa ikiwakabili.

Baada ya Yanga kuwasilisha malalamiko rasmi Oktoba Mosi, KIDAO alikataa Sekretarieti ya TFF kupelekwa suala hilo kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, na badala yake akafungua kesi dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela kwenye Kamati ya Maadili.

KIDAO na KARIA wamekuwa mawakala wakubwa wa agenda chafu za Simba kwenye soka la Tanzania huku wakiendesha Shirikisho watakavyo wao bila kujali taratibu na kila anayeonekana kuwahoji wamekuwa wakimtafutia utaratibu wa kumfungia.

#SisiNiMaShahidiTu
#hallaywsmm[emoji1241]
 
Wananikumbusha ya Malinzi, watoe majibu sasa ya kesi hiyo kwamba mkataba wa Morrison hauna mapungufu ili waaibike.
 
Mwakalebera ana kesi kubwa ya kimaadili kujibu, yeye si miongoni mwa waliopo kwenye mkataba lakini aliwezaje kupata mkataba wa Simba na Morison.
Halafu yanga walishasema wamefungua kesi Fifa mbona hawawashinikizi fifa kama wanavyowashinikiza Tff
 
Nimepita kariakoo nimekuta mashabiki wa upotolo wanaprint banner la platnum safari watahangaika sana kubadilisha mabwana
 
Mambo ya aibu kwenye mpira wetu tumeyazoea. Ilo Jambo la Morrison limewagharimu pesa nyingi sana Simba na baadhi ya watendaji wa kuu wa Tff wamepoteza uaminifu wao kwa vipande vya fedha sababu ya Morrison.
 
Haya ni malipizo. Mliwanyanyasa sana simba enzi ya yule kilaza wenu malinzi na genge lake la wahuni. Kudadadeq zamu yenu sasa kufiligiswa
 
Kosa lililofanywa na TFF wala Simba haihitaji kuishawishi au kukutana kwa siri na TFF, watalimaliza wenyewe TFF ili kulindana. Simba ilipeleka mkataba halali, ofisa akaupandisha usio
 
Mkataba wa awali ulikua na Mapungufu, yanini kutunza vitu vyenye walakini?
 
Tff waliona hoja yao haina mantiki mkataba unawahusu Simba na Morison na hakuna aliyelalamika upotolo wao wanahoji kama nani
 
Haya ni malipizo. Mliwanyanyasa sana simba enzi ya yule kilaza wenu malinzi na genge lake la wahuni. Kudadadeq zamu yenu sasa kufiligiswa
Kulipiza kwa kumkomoa huku unajitia hasara ni ujinga na upumbavu.
 
Usipanic ndugu, ndio dunia ilivyo. Hata ktk politics na mambo mengine mf kiuchumi HALI NDIO HIO HIO. Pambaneni na hali yenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…