Mkate tulionyang'anywa kwa vipigo wanataka kuturudishia kwa jina la maridhiano feki?

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,317
Reaction score
1,320
Nawasalimu wote.

CHADEMA tulikuwa na wabunge wengi kabla ya ukatili na chafuzi za yule mshamba, tukanyang'anywa kwa Hila, vipigo,vifo, vifungo na mateso.

Haya matatizo na uonevu tulifanyiwa na ccm Hawa Hawa wakiongozwa na jiwe/ kichaa.
Wametengeneza tatizo na wanajifanya kulisolve huu ni ulaghai mkubwa sana wa kisiasa CHADEMA tukikubaliana nao basi watatudharau kweli kweli.

Mtu mwerevu akikubaliana na ujinga kutoka kwa mjinga wote watakuwa wajinga tusikubali na tuseme hapana.

Maridhiano yawe ni juu ya kupata katiba Mpya na SI vinginevyo tusikubali kurudishiwa mkate ( waliouozesha) tulionyang'anywa kwa Hila kwani hiz ni blaa blaa tu.

Mwenyekiti wangu mbowe siasa hizi laini laini kwa ccm ni kupoteza mda . Hakuna maridhiano kati ya anayelia kwa maumivu na ayecheka kwa furaha ya kumsababishia mshindani wake maumivu.

Kama maridhiano ni kwa ajili ya kupewa wabunge hii HAPANA ccm wataendelea kutuchezea rafu wakijua wakituvunja miguu watatupa dawa ya kuchua na tutakenua.

Ikikufaa pia pumzika uenyekiti wa chama vijana wako waendeleze mapambano kwa nguvu na Kasi zaidi kwa mwendo huu ccm hatutawaweza kamwe.

CCM inahitaji siasa za jino kwa jino na sio za kupigwa Kofi shavu Moja na kumgeuzia linguine.

KATIBA MPYA, KATIBA MPYA KATIBA MPYA.
 
Ccm inahitaji siasa za jino kwa jino na sio za kupigwa Kofi shavu Moja na kumgeuzia linguine.
Mnataka siasa za mabavu wakati mkiambiwa muingie Barabarani hamtaki. Kina Mbowe wamelala jela wakipambania maslahi yenu ila walipoporwa ubunge na kupewa kesi za ugaidi sikuona aliyenyanyua hata mguu kumpa support zaidi ya mtandaoni tu.

Sasa kama wameona siasa za kibabe hazina tija sababu raia mmelala then waache watumie njia hiyo. Uzuri waliweka time frame kwamba kama hakuna reforms by October watajiondoa kwenye maridhiano.

So tuache maridhiano yaendelee ila pia tuna watu kama Lissu na Heche wanaozunguka kufanya mikutano yenye radicalism so twende kwa balance hiyo mpaka tuone njia ipi itazaa matunda.
 
Watu wako tayari kuingia barabarani mda na saa yeyote tatizo Huwa ni kauli za viongozi na pia wao nao wanapaswa wawe mbele. Sio kututanguliza sisi tu
 
Naunga mkono hoja, naunga mkono maridhiano, na namuunga mkono Mbowe kutumia kanuni ya "If you can't beat them, join them", Tanzania hakuna opposition ya kuishinda CCM, hivyo Mbowe amefanya uamuzi wa busara sana, to join them kwa mazungumzo ya maridhiano.

Baada ya kukubali maridhiano, kanuni ya "if you can't get what you want, just take what you get", kumaanisha ulitaka katiba mpya kabla ya 2025 ili tuweze kufanya uchaguzi huru na wa haki!. Muda uliobaki kabla ya uchaguzi wa 2025 ni a bit too little too late, hautoshi kutupatia katiba mpya, ila unatosha kubadili sheria ya uchaguzi na kuunda tume huru ya uchaguzi, hivyo uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki.

Hili mimemshauri Mama Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

P
 
Wee sema kisu hakijafika kwenye mfupa!
Kiongozi kama anabung'aa shika nafasi!
Sio pepo unaitaka ila kufa hutaki....
 
Huwa naukubali sana mwandiko wako wa kuuma na kupuliza.
Lkn pia mchakato wa katiba Mpya ulibaki sehemu mdogo sana ukiendelezwa ulipoishia hata kesho tunaweza kuwa na katiba mpya.pia huwezi kuwa na time huru bila katiba Mpya, maelezo Yako ni ya ku buy time tu hakuna kingine
 
Wee sema kisu hakijafika kwenye mfupa!
Kiongozi kama anabung'aa shika nafasi!
Sio pepo unaitaka ila kufa hutaki....
Hilo nalo tatizo la viongozi wetu Wana itaka Pepo halafu kufa hawataki.
Ndio maana tunamuhitaji lisu zaidi kwa sasa
 
Naunga mkono hoja, naunga mkono maridhiano, na namuunga mkono Mbowe kutumia kanuni ya "If you can't beat them, join them", Tanzania hakuna opposition ya kuishinda CCM, hivyo Mbowe amefanya uamuzi wa busara sana, to join them kwa mazungumzo ya maridhiano.

Baada ya kukubali maridhiano, kanuni ya "if you can't get what you want, just take what you get", kumaanisha ulitaka katiba mpya kabla ya 2025 ili tuweze kufanya uchaguzi huru na wa haki!. Muda uliobaki kabla ya uchaguzi wa 2025 ni a bit too little too late, hautoshi kutupatia katiba mpya, ila unatosha kubadili sheria ya uchaguzi na kuunda tume huru ya uchaguzi, hivyo uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki.

Hili mimemshauri Mama Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

P
Mzee wa kuuma na kupuliza [emoji16][emoji16]
 
Watu wako tayari kuingia barabarani mda na saa yeyote tatizo Huwa ni kauli za viongozi na pia wao nao wanapaswa wawe mbele. Sio kututanguliza sisi tu
Nani hayupo mbele? Siku Akwilina anauwawa mbona kina Mbowe walikua Frontline
 
Back
Top Bottom