Mkate wa Siha

Wingawinga

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
623
Reaction score
1,531
Kwa wale wahenga wenzangu wa Oysterbay na Masaki, mnakumbuka kipindi cha miaka ya 80, pale Morogoro stores, kulikuwa na duka lina uza Mikate ya Siha, kipindi hicho niko mdogo sana sikumbuki vizuri ila ninachokumbuka kama vile ilikuwa inapaikana mara moja kwa week na kulikua kama inagombewa.

Sijui sababu haswa ilikuwa ni nini kugombewa kihivyo na kwanini ilipatikana mara moja kwa weeki na je, Mkate wa Siha ulikuwa mkate unatengenezwa kwa nini haswa, sababu ulikuwana utamu a aina yake.

UPDATE.

Leo nime tambua jambo kuhusu MIkate ya Siha, siku zote nilidhani ni Mikate toka kwnye Bakery moja ndogo ya binafsi in Oysterbay na ndio ilikuwa ina bake hiyo mikate kwa ajili ya wateja wakazi wa Masaki, Oyesterby na Masasani na ndio maana nikasema Wahenga enzangu wa Masaki ana Oysterby ,sababu tulinunua hapo Morogoro stores in Oysterbay ( Pale ilipoPale maeno ya ilipo kuwa Maisha Club kwa wasio tambua Morogoro stores ) kumbe sivyo , Mikate ilikua Populary sehemu kubwa ya Tanania
 
Kwa wale wahenga wenzangu wa Oysterbay na Masaki , mnakumbuka kipindi cha miaka ya 80 , pale Morogoro stores, kulikuwa na duka lina uza Mikate ya Siha...
Kwangu, hiki ni kipimo, cha kuwajua wana JF ambao ni wahenga, na wanalijua JIJI toka enzi zilee za ma Ikarus! Enzi zilee za kufukuzana na magari ya NMC ili kununua unga!
 
Kwangu, hiki ni kipimo, cha kuwajua wana JF ambao ni wahenga, na wanalijua JIJI toka enzi zilee za ma Ikarus! Enzi zilee za kufukuzana na magari ya NMC ili kununua unga!
Nakumbuka Ikarus na mabasi ya Kamata, mabasi ya kamata yalikuwa hayo yalipita nje ya nyumbani kwetu , kipindi hicho niko mdogo , hausgeli wetu alikua ana penda kunitisha kama nilileta utundu kwamba ata niletea basi la Kamata nilinakate na nilikuwa na uoga mkubwa nikiona basi la Kamata.

Mabasi ya Ikarus nilikuwa ninayaona mjini zaidi ,kununua unga NMC hiyo sikumbuki vizuri ,pia nakumbuka mzee wangu siku ya Jumapili alikua haweze endesha gari, nadhani serikali ili zuia sababu ya ku save mafuta , tulikuwa na marafiki wa mzee wangu wanaishi Upanga, hivyo alikuwa akiwarudisha nyumbani kama wamekuja kututembelea nyumbani Jumapili ,basi alikuwa ana wafikisha mpaka maeneo ya Kenyatta Dr , pale wana shuka na kuetmbea kwenda Upanga sababu ukifika Slender Bridge gari ingekamatwa .
 
Siha maana yake ni afya njema, huo mkate ulikua ni wa NMC nadhani

Kula chuma hapo chini
 
Asante sana, je kwa sasa inapatikana hiyo mikate?
 
hiyo ndo miaka gari binafsi zilipangiwa muda wa kuwa barabarani hasa week end
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…