Mkate wa Siha

NdioπŸ˜‚πŸ˜‚, Mimi nilikuwa nakunywa na chai kwa style ya kuiloweka kwenye chai πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mimi hapo kuna Jam , yai na chai ya maziwa , ile TanBong nilikuwa siipendi na kipindi hicho sija jua Milo , nilikuwa ninadhani Milo ni kahawa na nilikuwa sipendi kahawa so Milo nilikuwa siitaki kabisa, ila baadae ndio nika ijua kumbe Milo ni tamu lol
 
Ilikuwa inagombaniwa sana jamani, tena huku kwetu ilikuwa inakuja asubuhi
Hata sisi ilikuwa inakuja asubuhi tena habari zina sambaa kwamba ime fika , huseboy aichelew nakua imeisha .
 
Na Jumapili ilikuwa ni kuanzia saa 8 ni marufuku kuendesha gari. Kuendesha gari Jumapili baada ya saa 8 ilitakiwa uwe na kibali.
Nakumbuka hiyo baba yangu ilikuwa na shusha wa gen alipo paswa warudisha majumbani kwo baada ya kuja kutusaliia nyumbani juma pili pale Kenyatta Dr, wate,bee hadi Upanga ,ili asikamatwe na police hapo Slender Bridge.
 
Hilo ndio nina hisi na ndio maana haipo tena sababu market yake haipo tena sababu kunamikate bora kila sehemu.
 
Siyo kama inawezekana ila ndiyo ukweli. Bidhaa nyingi zilikuwa adimu na hakukuwa na uchaguzi. Ukienda bar hakuna choice ya bia. Kama inatembea safari basi ni bar yote tena unaipata kama unajulikana. Kulikuwa na sehemu zinaitwa ''stoo bubu''. Hizi ni sehemu ambazo ulikuwa unaingia iwapo unajulika na kunywa bia. Mara nyingi ilikuwa ni vyumba vya kupanga na wauzaji wengi walikuwa wanawake. Ukienda ndani unaagiza kiasi kama tatu unaweka miguuni kwako kwa sababu muda wowote zilikuwa zinaweza kuisha.
 
Wow, kumbe ilipatikana mpaka miaka ya 87/88? mawazo yangu labda ilikwisha huko miaka ya 84, sikumbuki ,sante kwa taarifa.
 
Nakumbuka hiyo baba yangu ilikuwa na shusha wa gen alipo paswa warudisha majumbani kwo baada ya kuja kutusaliia nyumbani juma pili pale Kenyatta Dr, wate,bee hadi Upanga ,ili asikamatwe na police hapo Slender Bridge.
Salender Bridge ilikuwa ni sehemu mbaya sana sana kwa traffic polisi kukamata magari. Ukipita pale salama basi unashukuru Mungu.
 
dah , sikuwahifikiria kwanini watu walikuwa na story za kunua case na kuweka chini ya miguu, nilidhani ni ubishoo, kumbe ilikua uadimu wa vinywaji , asisee nilikuw amdogo kipindi hicho vitu vingi nilikuwa sivielewi ila ninaviona .
 
Salender Bridge ilikuwa ni sehemu mbaya sana sana kwa traffic polisi kukamata magari. Ukipita pale salama basi unashukuru Mungu.
Hahahahahahaha nakumbuka hilo , police walikua pale na enzi hizo kutoa rushwa ni ngumu na huwezi tumai mabavu kusema Mimi ni fulani .
 
Leo nime tambua jambo kuhusu MIkate ya Siha, siku zote nilidhani ni Mikate toka kwenye Bakery moja ndogo ya binafsi in Oysterbay na ndio ilikuwa ina bake hiyo mikate kwa ajili ya wateja wakazi wa Masaki, Oysterbay na Masasani na ndio maana nikasema Wahenga wenzangu wa Masaki ana Oysterby ,sababu tulinunua hapo Morogoro stores in Oysterbay ( Pale maeno ya ilipo kuwa Maisha Club kwa wasio tambua Morogoro stores ) kumbe sivyo , Mikate ilikua Populary sehemu kubwa ya Tanania na ilitengenezwa na shirika la umma.
 
Watu wa zamani walieliimika. Kwa sasa mkate wa Baharesa na super roof halina viwango, ndiyo maana tumeachie ugali uendelee. Hawana wapishi wenye viwango hadi serikali itakapo anzisha ushindani na viwanda vya mikate vya Ulaya.
 
HIyo ina weekana kabisa, quality ya vitu vingi imehuka sana , ina wezekana na hii moja wapo, sasa sijui kwanini hakuna mjanja aliyejaribu mimicking the recipe , hata kwa alio kuwa kwenye kitengo cha kuchanganya mazaga zaga , ili kitoke kitu kifananae na original kwa namna fulani , maana kama kweli ilikuwa na utofauti kihivyo basi ikija now itakua a big hit kwanye bakary industry .
 
Mikate ya Siha ilikuwa inatengenezwa na NMC pale Tazara, bekari alipewa AZAM na hstujui mitambo aliipeleka wapi, huenda viongozi wa CCM wanajua kwani ndio waliohujumu viwanda na makampuni yote isipokuwa cha majani ya chai tu.
 
Itabidi tuwahoji why wamefanya Chai isiwe fun kama zamani . lol
 
Ikarius nimeipanda sana lile roli aisrr lilikuwa likipita sehem kama ni posta likipita panabakia peupeeee, halikuwa na ruti maalum
 
Sahihi kabisa, ilikuwa inatengenezwa na NMC (National Milling Cooperation),ambalo lilikuwa shirika la umma. Yaani hiyo mikate ilikuwa mizuri mnoo (kwa sasa naweza kuilinganisha kwa mbaali na mkate wa SUPER LOAF [emoji506] from Kenya). Enzi hizo nikiwa Mburahati NHC ukiokota coins unaenda kununua Mkate wa Siha nusu na paketi ya maziwa ya KCC... Hawa NMC walikuwa wana magodown makubwa ya nafaka, bakeries etc kiukweli sijajua mambo yalikuja kuharibika kwa kweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…