Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imempandisha kizimbani Mkazi wa Mabwepande Jijini Dar es salaam, Shembiu Shekilaghe (38) akikabiliwa na mashtaka ya kutoa taarifa za uongo na kujifanya yeye ni Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete huku akijua sio kweli.
Wakili wa Serikali, Salma Jafari amesema hayo jana September 23, 2024 alipokuwa akimsomea Mshtakiwa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa ambapo amedai Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka 14 huku mashitaka ya kwanza ya pili na tatu yakiwa ni kutoa taarifa za uongo.
Amedai September 02,2024 Mshtakiwa akiwa katika eneo lisilojulikana ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa taarifa za uongo kupitia Akaunti ya mtandao wa kijamii ya Facebook yenye jila la Mrisho Jakaya Kikwete akisema “Ukiweka akiba ya 49,000 utapata mkopo wa laki tatu marejesho ni Tsh. 30,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 10”
Amedaiwa katika tarehe hiyohiyo kupitia akaunti hiyo pia alitoa taarifa ikisema “Ukiweka akiba ya 59,000 utapata mkopo wa Tsh. 400, 000 marejesho ni Tsh. 40,000 kila mwezi kwa muda wa miezi 10, ukiweka akiba ya Tsh. 69,000 utapata mkopo wa laki tano marejesho ni Tsh. 50,000 kila mwezi kwa miezi 10”
Mashtaka mengine ni ya kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Mtu mwingine ambapo inadaiwa kuwa September 3,2024 katika eneo la Mji mpya Mabwepande alikutwa akitumia namba ya simu iliyosajiliwa kwa majina ya Matias Ngowi, Modesta Marumi, Jane Mhanga, James Zephania na Amini Omary na kujipatia fedha kiasi cha Tsh. 100,000 kutoka kwa Samson Mwandawila kwa kudai atampatia mkopo wa Tsh. 800,000 huku akijua si kweli na kujipatia fedha Tsh. 100,000 kutoka kwa Rudi Maduka akidai atampatia mkopo wa Tsh. 1000,000 kupitia taasisi yake ya Jakaya Kikwete foundation.
Baada ya kusomewa mashtaka yake mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na Wakili Jafari amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo ameiomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kusomaa hoja za awali, Hakimu Magesa ameahirisha kesi hiyo hadi October 10, mwaka huu kwa ajili ya kusomwa hoja za awali na Mshtakiwa amerudishwa rumande baada ya kukosa Wadhamini.