Mkazo Zaidi Uwekwe katika Ujasiriamali.

Reckon Master

Member
Joined
Nov 7, 2018
Posts
9
Reaction score
5
Neno ujasiriamali si, neno geni miongoni mwetu na kumekuwa na dhana nyingi sana kuhusiana na ni nani mjasiriamali na ni nani ambaye sio mjariamali.

Mjasiriamali katika dhana ya kisasa ni mtu ambaye ni mbunifu au mwanamaendeleo (developer), ambaye anaziona fursa na kutumia nguvu zake, muda wake, na fedha zake kubadilisha fursa hizo kuwa wazo bora la kibiashara ambalo linaweza tekelezeka na kuleta au kumletea manufaa baadae.

Ujasiriamali una faida kubwa kwa mtu mmoja mmoja na mpaka kwa taifa kwa ujumla. Hivo basi, ni lazima mkazo zaidi uweke katika kuchochea ukuaji wa shughuli za kijasiriamali. Mkazo uweke zaidi kwenye ujasiriamali wa vitendo na sio ule wa maneno mengi. Elimu juu ya masuala yahusuyo ujasiriamali iboreshwe zaidi ili ari na uthubutu wa kufanya ujasiriamali uongezeke zaidi.

Ni lazima tuwe wabunifu kila iitwapo leo. Ubunifu na ujasiriamali vinaenda pamoja. Hauwezi kuwa mjariamali mzuri kama utashindwa kuboresha ubunifu wako.
 
Wote wakiwa wafanyabishara,mafundi wa kujenga vitu ili uviuze utavipatia wapi?
 
Wote wakiwa wafanyabishara,mafundi wa kujenga vitu ili uviuze utavipatia wapi?
Biashara inaanza pale ambapo watu wana mahitaji ambayo hayajatamizwa na uwezo na nia ya kutaka kutimiza mahitaji hayo wanao (uwezo wa kununua). Kwa hiyo watu (soko)wa kuwauzia wapo na watakuwepo tu. Watu tuna mahitaji tofauti na utofauti huo wa mahitaji ndio unaoleta sababu ya kutaka kubadilishana vitu ili kukidhi mahitaji yetu mfano nguo vs fedha
 
Biashara inaanza pale ambapo watu wana mahitaji ambayo hayajatamizwa na uwezo na nia ya kutaka kutimiza mahitaji hayo wanao (uwezo wa kununua)

Sio lazima kuwe na uhitaji!

Unawezajenga "uhitaji" jamii ikaelewa somo wakazalisha "uhitaji"!

Kama ni kuangalia "uhitaji" kwanza,basi internet,umeme,etc visingevumbuliwa!

Kwa hiyo watu (soko)wa kuwauzia wapo na watakuwepo tu
Wanaweza wasiwepo pia!

Unaweza kudhani wapo kutokana na "assumed" au 'illusions" zako, kumbe in reality hakuna hilo soko unalodhani lipo japo reasearch na numbers zote kwako zinasema lipo!

Watu tuna mahitaji tofauti na utofauti huo wa mahitaji ndio unaoleta sababu ya kutaka kubadilishana vitu ili kukidhi mahitaji yetu mfano nguo vs fedha
Hii ni concept basic kabisa ya human trade from the ancient times up to now!
 
Wote wakiwa wafanyabishara,mafundi wa kujenga vitu ili uviuze utavipatia wapi?
Ujaeleweka hapo mwisho, ila ujasiriamali sio ufundi wa kujenga vitu nineo controversial linafiti kila idara na watu wataendelea kuishi kama kawaida.

Mfano mfanya biashara aliyewekeza kwenye kiwanda cha kujenga chupa za plastic anamuuzia MO, wakati huo MO naye ni mfanyabiashara atamuuzia juisi uyu mwenye kiwanda.
 
Mifano yako mbona sio validity kwakuangalia uhitaji Internet isingekuwepo | kabla ya kiwepo mboba waliangalia uhitaji mbalimbali mawasiliano nk.
 
Ujaeleweka hapo mwisho, ila ujasiriamali sio ufundi wa kujenga vitu nineo controversial linafiti kila idara na watu wataendelea kuishi kama kawaida.
Yaani human beings wote wakiwa wafanyabiashara,jee mafundi wa kujenga vitu viweze kutokea ili viuzwe watatoka wapi?

Umenielewa?

Mfano mfanya biashara aliyewekeza kwenye kiwanda cha kujenga chupa za plastic anamuuzia MO, wakati huo MO naye ni mfanyabiashara atamuuzia juisi uyu mwenye kiwanda.

Hicho kiwanda ka-design nani,kajenga nani,mashines kajenga nani,nani anaziendesha mpaka ukapata final product ya juice mkaniuzia mimi?

Ni mafundi,engineers,sasa wewe unaona hawa ni hovyo wanatakiwa wawe wafanyabishara as they are!

In a long term hiyo ni myopic view!
 
Mifano yako mbona sio validity kwakuangalia uhitaji Internet isingekuwepo | kabla ya kiwepo mboba waliangalia uhitaji mbalimbali mawasiliano nk.

Hivi unajua historia ya internet?

Unajua historia ya umeme ulipotokea?

Wewe ni engineer?

Kama sio,ni heri unyamaze sio unabisha vitu huvijui!
 
OK naona hili swali lishaulizwa hata mala 100000 humu JF, jibu ni hili.

Kutoa elimu ya ujasiliamari haina maana kwamba wote wataifata lakini hii haimaanishi isitolewe na wanaopewa watoa hoja kwamba sio lazima tuwe wote wajasiliamari, hili jambo linaanzia mbali.

Tunajua kuna pepo na moto, ila ujumbusho ni jambo jema kwamba tumuabudu Mungu tusiingie motoni ila uwezi sema eti siolazima wote tuingie peponi motoni ataingia nani, na nikweli kuna watu hawatafata huwo ukumbusho.

Nirudi kwenye point, ukumhusho wa ujasi ni muhimu kwasabau tukiwa watu wengi wanaojiweza watalipush taifa mbali ila sikwamba wote wataingia uko kwenye wajasiliamari mkuu hata uwahimize watu kwafimbo.

Mwisho
Huitajiki kutoa hoja kama hiyo
 
Kutoa elimu ya ujasiliamari haina maana kwamba wote wataifata lakini hii haimaanishi isitolewe na wanaopewa watoa hoja kwamba sio lazima tuwe wote wajasiliamari, hili jambo linaanzia mbali.
kama sio lazima kuifuata,yanini usome kama sio kupoteza muda?

Kwanini usisome unavyovipenda na utavifanyia kazi?

Au kwa kifupi,kwanini tusisome vitu tuvipendavyo?

Tunajua kuna pepo na moto,
Pepo na moto unaijua wewe!

Kwavile wewe ni judean christian unaamini on heaven and hell unadhani dunia nzima tunaamini huo upumbavu!

Usiwe una-assume vitu!

Ungeanza kwa kuandika "According to my religious belief........."

ila ujumbusho ni jambo jema kwamba tumuabudu Mungu tusiingie motoni ila uwezi sema eti siolazima wote tuingie peponi motoni ataingia nani, na nikweli kuna watu hawatafata huwo ukumbusho.

Muabudu Mungu wewe!

Usilazimishe the rest of the population!

Unaamini Mungu unaamini wewe,sio wote!

Jiongelee kwa niaba yako binafsi!

Nirudi kwenye point, ukumhusho wa ujasi ni muhimu kwasabau tukiwa watu wengi wanaojiweza watalipush taifa mbali ila sikwamba wote wataingia uko kwenye wajasiliamari mkuu hata uwahimize watu kwafimbo.

Ni vizuri umetoa maoni yako....na mimi nina yangu...na wote tuko poa!
 
Hata hao mafundi pia ni wajasiriamali kwa sababu wanatumia ubunifu wao kutengeneza vitu na kuviuza

Si kweli in a sense!

Kama definition ni hiyo,kila mtu duniani ni entrepreneur,wether ni daktari,mpishi,mvuvi,mganga,muhubiri,mtangazaji,etc

Mzee,hizi definition mnazishusha mno mpaka matopeni!

Hebu tuwe serious kidogo!
 
Si kwelu in a sense!

Kama definition ni hiyo,kila mtu duniani ni entrepreneur,wether ni daktari,mpishi,mvuvi,mganga,muhubiri,mtangazaji,etc

Mzee,hizi definition mnazishusha mno mpaka matopeni!

Hebu tuwe serious kidogo!
No si kila mtu ni mjasiriamali bali yule anayefanya ubunifu akatengeneza kitu au huduma na ikampatia pesa.
 
Kwanini watu wanaogopa kuwa wajasiriamali akati wanajua taratibu zote za kuwa mjasiriamali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…