Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka 30

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
MWANAMKE mwenye umri wa miaka 60, mkazi wa Kibaoni mjini hapa, amewavunja mbavu wasikilizaji wa kesi katika Mahakama ya Mwanzo Ipembe, baada ya kumjibu Hakimu kuwa kijana aliyemfikisha mahakamani hapo si mwanawe bali mumewe.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo Asha Abdallah anamshitaki mumewe, Kiemi Itambu (30), kwa kumwibia Sh 30,000 alizokuwa ameficha chini ya godoro.

Wawili hao wakiwa kizimbani jana, Hakimu Hosea Mkude alimwuliza mke: “Kwa nini wewe bibi unaolewa na kijana ambaye ana umri wa mwanao, huoni aibu?

Asha alijibu: “Mheshimiwa, huyu ni mtoto kwa mama yake aliyemzaa, kwangu ni mume wangu halali ambaye ananitimizia mahitaji yangu yote muhimu.”

Kama vile jibu hilo halikutosha, Asha aliendelea ‘kumpasha’ hakimu: “Kwanza kwa taarifa yako, wako wanawake wengi tu hapa mjini walioolewa na vijana, tena wengine wana vijana wenye umri unaofanana na wa wajukuu zao. Sembuse miye?”

Majibu hayo yalisababisha watu waliojazana kwenye chumba hicho cha Mahakama, washindwe kujizuia na kuangua vicheko.

Ilidaiwa mahakamani hapo, kuwa mshitakiwa Kiemi alitenda kosa hilo Novemba 3, saa mbili asubuhi Kibaoni mjini hapa.

Asha alidai mahakamani hapo kuwa mumewe amekuwa na tabia ya kumwibia Sh 100, 200 na 500, lakini safari hii alivuka mpaka kwa kuiba Sh 30,000 ndiyo maana akaamua kumfikisha mahakamani.

Mshitakiwa alikana mashitaka na yuko nje baada ya kujidhamini mwenyewe kwa ahadi ya kutoa Sh 50,000 hadi Novemba 15 kesi hiyo itakapotajwa.

Source: HabariLeo | Mke (60) amshitaki mume mwenye miaka 30
 
Duhh ama kweli ng'ombe hazeeki maini
Jamaa kadokoa 30,000/- wife kaamua kumpeleka kwa pilato
 
Huyo hakimu alipata majibu yanayomfaa.

yeye imemuhusu nini kaolewa na nani?!
 
Reactions: SMU
Huyo hakimu alipata majibu yanayomfaa.

yeye imemuhusu nini kaolewa na nani?!

Hakimu alikuwa mnoko tu watu wamependana na wanaridhishana ndo kikubwa katika mapenzi
 
hahahhaaaaa hakimu alikuwa anaenda nje ya mada akaipata fresh. Sasa endapo mume akapatikana na hatia na kufungwa, je akitoka huko hiyo ndoa bado itakuwepo kweli au kuna sheria inayosema lazima uendelee na ndoa yako ukitoka gerezani endapo mwenza wako ndie aliyekupeleka huko?
 

Mlalamikaji anaweza akakosa imani na hakimu kabisa
 
Safi sana bi aisha abdalahh!!! Umenipashia hakim hadi kapashika.....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…