Mke akikuzidi elimu,kipato penzi linaweza kudumu?

Joined
Jul 13, 2011
Posts
64
Reaction score
8
By Herieth makweta.
MARA nyingi wengi tumekua tukichukulia masuala ya kiuhusiano tofauti na vile ilivyo kawaida
Siku zote wanawake hujitahidi kutafuta wanaume wenye vipato vyao na wangine pia kutafuta wale waliowazidi kielimu. Hata hivyo wanaume wengi wamekua waoga kua na wanawake waliowazidi kielimu na wengine wakiogopa wale wenye vipato vikubwa kuliko wao.
Katika kutafuta usawa wa kifikra,"Mwanamke akikuzidi elimu na mshahara wengi hufikilia wataachwa au kunyanyasika je ni kweli ?"
Nawasilisha wana MMU
 
tatizo ni kwamba mwanaumme akiona amezidiwa kiuwezo na mke wengi wanajifeel inferior anaanza kuishi kwa kutojiamini na kwa kujidefend soo conflict zinaanzia hapo
kama mwanamme ataweza kurelax ndoa itadumu
 
no clear cut answer on this question na sio appropriate ku-generalise kwamba wanaume watareact in the same way... all in all, penzi linaweza kudumu kama limejengwa kwenye msingi imara wa upendo na kuheshimiana bila kujali kuzidiana kwa elimu au kipato
 
Mimi kuzidiwa kipato na elimu sio tatizo.As long as the woman in question respects me and plays her role as a good wife is supposed to,no problemo.The relationship can be healthy,afterall i get to have someone who can help me in financial matters incase the downtimes kick in.
 
Nakuwa baba wa nyumbani
Napika na kupakua kwa raha zangu.
 
Kwa mazingira na wanawake wa kitanzania ndo nyingi ambazo mwanamke ana kipato na madaraka wanaume wananyanyasika sana na baadaye ni divorce
 
Nafikiri suala c elimu ya juu au fedha kumzidi mwanaume, suala ni mhusika anaelewa nini kuhusu mapenzi/upendo. Wahenga walisema 'mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo' . Wapo baadhi ya wanawake wenye fedha/kipato kikubwa na elimu nzuri na wanaishi na waume wenye vipato/elimu ya wastani lakini maisha yao yapo poa tu.

Zipo ndoa ambazo zimekuwa na matatizo kwa mitizamo ya kuwa na tofauti ya kipato/elimu baina ya wanandoa, lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuna tatizo lipo kwa wanaume kuanza kutojiamini hasa wale wanaume wababe( wao hawataki ushauri na wanajua kila kitu) mwanamke akitoa wazo 2 utasikia, kuwa na hako ka digree 2 umeshaanza kujifanya kichwa na nyumba.

Mwanamke akishauri kufanya jambo la maendeleo kwa kuchangia fedha ataambiwa anapewa na bwana zake/anahongwa na boss. Mwanamke asipokuwa mvumilvu(japo kuna kiwango cha mwisho) ndoa lazima ivunjike au iwe wodini kila siku.

Kuna tatizo la kuigiza ili kufikia matarajio kwa baadhi ya wanandoa (hasa wanawake), mwanamke anampenda mwanaume na kuolewa naye kwa sababu alimwahidi kumsomesha au kumfungulia mradi wenye kuingiza kipato kizuri. Wanawake wa namna hii baada ya kufanikiwa kufikia matarajio yao hubadilika mifano ipo mingi (mi nanfahamu jamaa yetu aliyemwendeleza mkewe aliyekuwa anatamani kuwa daktari baada ya kuwa clinical officer alianza kucheat na mwanaume mwingine ( huyu sasa ndo amempenda baada ya kufikia matarajio) baada ya migogoro ya muda mrefu mumewe akaamua kubwaga manyanga.
Hebu chunguza baadhi ya wanawake wenye biashara kubwa hali za ndoa zikoje
 
linaweza kudumu pale utapokubali kuvaa wajibu wa mke na yeye kubaki kuwa kama baba, it will work smoothly. Huna sababu yakujidai kidume wakati bajeti inamtegemea mama..
 

Ila wanawake wingi wenyekipato huwa wanamanyanyaso mengi,walio wengi wanaishi peke yao
 
linaweza kudumu pale utapokubali kuvaa wajibu wa mke na yeye kubaki kuwa kama baba, it will work smoothly. Huna sababu yakujidai kidume wakati bajeti inamtegemea mama..

Kaka lazima nitoke nduki hapo kwani hakuna mapenzi tena!
 
Kuna suala la inferiority ambalo linaweza kuibuka hapo na mwanaume akawa anajihisi kudharauliwa, japo pia inaweza kuwa ni kweli anadharauliwa. Ila kiuhalisia suala hilo linategemea na watu wenyewe hakuna formula kwamba ikiwa hivi ni lazima itakuwa hivi hapana.
 

Mapenzi ya kweli, hayaangalia kipato au life status ya mtu. Thanx
 
nawashangaa wenzangu wanaopata inferiority complex....mi binafsi ningefurahi kinoma,nisingefanya hata kazi...ningekua house husband.mambo ya kupika,kuandaa watoto kwaajili ya shule,kutafuta house grl anayechakachulika siyo hawa wabaya wanaotutafutia sa hizi....playstation and alcohol siku nzima
 

Hakuna ukweli wowote na hili,
Mifano mingi iko, ndoa inazidi kudumu kwani kipato cha familia kinakuwa poa, hivyo kupunguza maugomvi yale common kuvunja ndoa, mfano kila siku kukabana kabali mume kutoa hela ya mboga, au pesa za nguo ya sikukuu kwa watoto au............
Na wanaume wengi siku hizi wameligundua hili na hivyo kukwepa kuoa "magoli kipa"
 
Inategemea na mwanamme vile vile,mwanamke unaweza kua na kipato cha juu na ukawa na adabu zako,mume ndioa akaanza vituko ukiuliza ndio anaanza ohh kwasababu wewe ndio unauwezo kuliko mimi hayaoni mapungufu yake......
 
katka hili kila mtu anatakiwa kujitambua yeye ni nani bila kujari vipato maana hapo kwenye kipato ndiyo mambo huanzia kuharibika lakini kama kila mmoja ataonyesha mapenzi ya kweli hili halitakuwa nauzito katika ndoa kila mmoja atafurahia tu maisha bila kujari kama mwenzake anamzidi pesa au laaaaaaaaaa
 
hakuna tatizo katika hilo,mi nachojua ambacho ni cha msingi ni maelewano na kuheshimiana tu.elimu na pesa hivina nafasi katika ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…