Thank you King'asti kwa ushahidi...mara nyingi wanaume wanakulaga kona. Ni wanaume wawili tu kati ya discordant couples karibu 30 nilizowahi deal nazo walibaki na partner. Kuna mmoja mkewe aligundulika baada ya kujifungua, aliumwa sana..mumewe alikuwepo 24/7 akimhudumia mama na mtoto mchanga japo ndugu walikuwa wanachonga mpaka kutaka kunihonga kama Daktari nimshauri ndugu yao aachane na huyo mama, nikawatimua kama mbwa! unfortunately yule mama alifariki kama miezi 7 baadae, jamaa is my friend mpaka sasa, he is still -ve and thank god the kid is now 4 years and -ve!
Couple nyingine walikuwa walokole walitaka kuoana, madad akawa +ve na mkaka -ve....lakini huyu mkaka jasiri alikubali kumuoa akiamini yesu atawapigania..akaoa na nikawafuatilia wakifuata masharti na aliendelea kuwa -ve kwa miaka mi2, then wakataka kuzaa...nikawashauri wafanya in-vitro frtilization (IVF), yai linarutubishwa bila tendo la ndoa...kaka akakataa, akasema atampa mkewe ujauzito kwa njia ya asili (tendo la ndoa), series of counselling zikashindwa kutokana na imani yake ya kiroho. Akajaribu kumpa mimba mkewe lakini haikuwa rahisi kihivyo, wakarudia na kurudia, na miezi 6 baadae kaka akawa +ve. Tulipompa majibu alichanganyikiwa na akapotea sikumuona tena clinic, na jitihada zangu kumtafuta kwa contact nilizokuwa nazo hazikuzaa matunda...it is one of my saddest story in practising clinical medicine.
It is a challenge kwa kweli, hasa linapokuja suala la kuzaa. King'asti hiyo couple yako watianaje mimba 3?