Kujipodoa wakati wa kwenda kazini, au kutoka ni kawaida kwa wanawake wengi. Na wakati mwingine huwa ni tabia na mazoea ya mtu kupenda kujipodoa.
Linapokuja suala la mavazi, hapo inategemeana na tabia utashi na umbile la mtu. Kuna maumbile mengine mavazi mengi utakayovaa yataonekana kama ya uchokozi. Hata hivyo hii haina maana mwanamke avae mavazi mafupi sana, au aachie kifua wazi, au ya kubana sana kuonyesha mkato wote wa mwili. Kama mchumba wako anavaa mavazi ya uchokozi ambayo wewe huyapendi, mshauri aache, hata kama yeye anafurahia kuvaa hivyo bila kujali wanaomuangalia. Naamini atakusikia, ukiona mnashindana kuhusu mavazi na kuzidisha vipodozi, sogeza mbele tarehe ya harusi na uendelee kumchunguza bila shaka utagundua mengine.
Kitu kingine chunguza tabia ya mchumba wako ambapo itakuwa rahisi wewe kumshauri na kujua la kufanya.