Kwa hiyo kama unafikiria kuoana na mwanamke imara sana kiuchumi, au kielimu, sikushauri uache au uendelee, maamuzi ni yako, ila jitahidi kuhoji ni kwa nini hajaolewa�hasa kama ana umri wa miaka 35 na kuendelea.
Najua atakueleza sababu nyingi za kuachana na wapenzi wake wa zamani, nyingi zitaonyesha alioachana nao ndiyo walikuwa na matatizo.
Tafakari kwa makini zaidi, hasa kama alishawahi kuwa na mtoto au watoto au kuwepo kwenye ndoa. Kuwa kwenye ndoa ni raha lakini ni hatari kama unakuwa kwenye ndoa na mtu ambaye hakupi amani.