Under-cover
JF-Expert Member
- Nov 13, 2023
- 1,834
- 3,042
Your browser is not able to display this video.
VIDEO Francis Butoto anayesadikika kuwa na miaka 64 Mkazi wa Kijiji cha Kishanda kata ya Kibare tarafa ya Murongo wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameuawa na kufukiwa kwenye shimo la choo kilichokuwa kinatumiwa na kijana wake, ambapo watuhumiwa wanne wanakamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo akiwemo mke wake.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera SACP Brasius Chatanda amesema kuwa walitekeleza mauaji hayo February 22, mwaka huu na chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na mgogoro wa mali za familia ambapo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Frola Bitakalamile (42) ambaye ni mke wa marehemu, George Bitaka (52), Detric George (19) na Christopher Bitakalamile (30).
Hata hivyo Kamanda amesema kuwa "baada ya tukio hilo na watuhumiwa kukamatwa wananchi wakazi wa eneo hilo walijichukulia sheria mkononi na kwenda kuharibu Mali za Bitakalamile, hata hivyo na wao wanasakwa na jeshi la polisi na orodha yao tayari tunayo". #EastAfricaTV