Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,375
- 6,958
Wanao badili majina wanamatatizo gani kama siyo muhimu, au nini kinacho wafanya wabadili?Mie naona halina umuhimu wowote hata ningekuwa mie siwezi kutumia jina la ukoo wa mume,
Watoto wetu ndo watatumia jina sio mie😉
Ni makubaliano (maridhiano) tu baina ya wawili hayaongozwi na sheria wala amri amasivyo kingeongezewa kwenye kiapo cha ndoa 'Bibi flani bin Flani, uk tayari kubadili jina la baba yako, uliache/kulikana na kutumia la mumeo?' watu wanacomplicate maisha utadhani hawana shughuli za kufanya ah!!
Mnapendana, mnaheshimiana na kuaminiana inatosha!! But if he think it is that necessary basi atake trouble ya kubadilisha (maana ile process ya kubadili hadi vyeti inakera).
Mie naona halina umuhimu wowote hata ningekuwa mie siwezi kutumia jina la ukoo wa mume,
Watoto wetu ndo watatumia jina sio mie😉
huyo dada yupo sahihi mimi naona coz hapo alipo kapitia shule kibao na pengine vyuo mbalimbali, vyeti vyote vina majina ya baba yake mzazi na wakati anaajiriwa si alipeleka vyeti vya shule vyenye jina la baba mzazi sasa jamaa ana hofu gani na jina? haamini km atakuwa wake km jina lake halitatumika? aache ugomvi bana tena siku hizi wanawake wengi hawapendi sana kuitwa mrs fulani, wanapenda tumia majina yao ya kwanza utasikia miss esther, je ingekuwa namna hiyo jamaa si angerusha ngumi
Hahaaahaaa kama ulikuwepo!Mwambie jamaa agombenia urais na mungu akimsaidia apate utaona ,wife wake atataka kubadili jina
aaaaaaaaaaah, sio lazima jamani, kwani kubadili jina na kufuata la mumeo ndio kunaongeza nini ama kupunguza nini? Cha muhimu mnapendana, mnaaminiana, na pia kuheshimiana, basi! Jina halisaidii kitu, libadilishwe ama libaki la baba, hakuna kitakachopungua, wala si lazima!
Ndoa za siku hizi ni balaa sababu za kutokutumia jina la mumeo ni kuwa siku mkachana yuko kivyake na pia mke amejishkiza tu kwako au anaona jina la babake linalipa kuliko surname yako ndio ndoa zetu siku hizi maana kuna rafiki yangu mkewe aligoma kutumia jina la mume wake ampaka kidogo waachane. Mume akaamua kuwa mpole lakini leo hii kila wanachofanya mpaka risiti za kununulia vitu kama saruji, mbao n.k mke anaandikisha majina yao wote wawili...Ndoa za leo ni kindoano ndoano tu na kimaslahi zaidi
Mwambie jamaa agombenia urais na mungu akimsaidia apate utaona ,wife wake atataka kubadili jina
Yeah sure ndoa za siku hizi inabidi uwe mguu ndani mguu nje haziaminiki chochote chaweza tokea wakati wowote na trend yake yaweza kuwa hivi;Huyo mwanamke ndio wale wenye akaunti mbili za siri ambazo mume hajui! Yaani mnaishi kimachel machale tu ndani ya nyumba!