Mke: Kajala niachie mume wangu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Wakati Diva wa Filamu Bongo , Kajala Masanja ' Kay ' akielezwa kuwa mambo yake hivi sasa yako kwenye mstari kwa kusajili Kampuni yake ya mambo ya Sinema , mwanamke aliyejitambulisha kwa jina moja la Pamela ameibuka na kumtaka muigizaji huyo kuacha kumfuata mume wake , Amani lina data kamili .

Mwanamama huyo , anayefanya kazi ' nzuri ' katika Shirika moja kubwa Nchini , aliliambia gazeti hili kuwa Kajala , amekuwa akitembea na mumewe aliyemtaja kwa jina moja la Tanaluza ambaye kwa sasa yuko ndani katika gereza la Keko kwa kosa ambalo alikataa kulitaja. "Jamani namtahadharisha Kajala , asije kunikuta pale, patakuwa hapatoshi , yeye si hodari wa kwenda kuangalia waume za watu , awe na haya , aende Ukonga akamuangalie mumewe , ushauri wa bure nampa , " alisema Pamela kwa jazba .

Alisema anazo taarifa kuwa Kajala alikuwa akitembea na mumewe kabla hajapatwa na matatizo na baada ya kupelekwa Keko Gerezani , amekuwa akienda hapo kwa kujifichaficha, kitu ambacho alisema siyo kizuri kwa sasa, kwani anaweza kumsababishia mumewe matatizo zaidi .

"Huyo ni mume wangu , ananihitaji kwa hali na mali sasa hivi , nisije nikaacha kwenda kwa ajili ya Kajala , kama aliwahi kumpangishia Nyumba ya kifahari na kumnunulia Gari, ni huko huko , sasa hivi anahitaji kuwa na mimi mkewe , kwanini yeye asiende kwa mume wake na yeye si amefungwa ?, " alihoji Pamela .

Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mke , Gazeti hili liliingia mtaani kwa nguvu kumsaka Kay , ambaye mume wake , Faraja Augustino amefungwa Jela miaka saba kwa kosa la utakatishaji fedha na kufanikiwa kumpata kupitia simu yake ya mkononi. "

Mimi mbona simjui huyo mwanaume, wala sijawahi kufika huko Keko , kama anatafuta umaarufu kupitia jina langu aseme , asinisingizie , " alisema Kajala baada ya kusomewa mashtaka yake , majibu ambayo licha ya kuyaheshimu , lakini gazeti hili linaendelea na uchunguzi wake ili kubaini ukweli zaidi .
 

Attachments

  • 1421330894506.jpg
    53.7 KB · Views: 593
EEH kajala na wewe kiboko , unaacha kwenda segerea kwa mumeo unaenda kwa mume wa mwenzio , nyooo
 
Hahahahah

Huyu kiazi kweli

Anaacha kwenda kumtembekea mumewe anaenda kwa mune wa mwenzie???

Au ndio asante kwa brevis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…