Mke kazira kutumia gari: Ushauri please


Possible umemsimanga nalo acha alizire! Ingekuwa mimi ingekuwa mie ingeambatana nakugonga BAN YA 2 WEEKS, NO DUDU hadi unajiju!
 
mkuu,hiki kisa chako kimenifundisha kitu,
nilikuwa na mpango wa kumnunulia wife usafiri(baiskeli ya gia) awe anaendea kazini nahc ataleta dharau kama hizi,ishamkost,ndo hapati tena kitu,na hta akinunua mwenyewe nauza!
 
kama shughuli zake ziko kariakoo mwekee alarm sababu kule watu wako na shughuli mbalimbali, wengine wanawaaga wake zao wanaenda kazini, kazi zenyewe ndio hizo za kuiba, wakipata upenyo wanaiba, pia tafuta njia nzuri ya kumwambia mkeo asione unamsimanga, kwani gari si yake na ww una yako?
 

WEll said hapo kwenye RED. Watu ambao huwa wakikosolewa wanasema wanaonewa (wanatumia maneno kama unanidharau, unanisimanga, unajisikia sana nk) wanasumbuliwa na a low self esteem; makuuzi yao hayakuwajengea kujiamini na kujithamini; mara nyingi wanakuwa paranoid...kila wakati wanahisi kuonewa na mara nyingi ni wepesi kuanzisha ugomvi wa maneno...Nyani mzee, naamini hili si tukio pekee...lakini nakushauri kwa kuwa ni wife you need to understand her; ni weakness ambayo ina mizizi mirefu so learn to live with her.
 
Sokwe bana, umenifurahisha sana, ila unachosema ni kweli mkuu!
 
shukuru Mungu hawajamvamia kuchukua gari lote na kumpiga yeye, wewe mtengenezee tu sio kulalama, wanawake ndivo tulivo
 
shukuru Mungu hawajamvamia kuchukua gari lote na kumpiga yeye, wewe mtengenezee tu sio kulalama, wanawake ndivo tulivo
Mwanamke katokana na ubavu wa kushoto wa mwanaume na sifa ya ubavu
ni kuwa umepinda, kwa hiyo mwanamke AMEPINDA.
 

huyo ana yake..... kama unabisha weka magari ndani na usimpe ikifika wiki utajua kila kitu
 
huyo ana yake..... kama unabisha weka magari ndani na usimpe ikifika wiki utajua kila kitu
Solution si kuweka ndani, hiyo gari amkabidhi HOUSE GIRL ili apime
vizuri kina cha maji!
 
Ndugu yangu Nyani Mzee,

Wake zetu hawa ndo hivyo, ni handle with great care. Yaani hiyo situation yako nimeshakumbana nayo mara kibao! Solution ya leo haitafanya kazi kesho. Ila kama wengi wanavyosema hapa mwanamke anakuwa na ile feeling kwamba na yeye ni bosi hivyo hatakiwi kusemwa semwa. Lakini vile vile mwanamke mwenye udhaifu fulani kama kutojali mali, usahaulifu sana, kukosea kitu fulani anajenga defence mechanism.

Wanawake wengi kutokana na aina ya malezi yanayopata utotoni, wanakuwa wakubwa huku wakiwa na vitabia vingi vya kitoto. Hiki kitabia ni mojawapo. Yaani amefanya makosa, hataki akosolewe, akikosolewa yule anayemkosoa ndo anamuona mbaya wake. Halafu hapo lazima kuna watu wa nje (hasa mashosti zake) anawasimulia wanampa ya kumpa.

Mie msimamo wangu ni kuwa ulichofanya ni sahihi. Lazima umuoneshe kama anachofanya ni makosa na inatakiwa awe mwangalifu. Alichotakiwa kufanya ni kukuomba umpe ushauri afanyeje asiwe anaibiwa na ajaribu mbinu utakazompa. Lakini kwa mwanamke kukubali mbele ya mme wake kuwa amekosea; hasa kosa lenyewe likiwa hili la kujirudia rudia, anaona ni udhaifu. Sababu kubwa ni kuwa wanawake mara nyingi huwa wanaongea sana na marafiki zao mambo yao ya ndani mno na mara nyingi wanashuliwa vibaya.

Najua atalalmika kuwa una mnyanyasa, una gubu, n.k. Lakini usipofanya hivyo itakuwa mbaya zaidi. Ni afadhali aone unamnyanyasa kwa muda mfupi hatimaye atagundua tu kuwa kosa ni la kwake.

Mwanamke hata siku moja hatakubali kujishusha kwa mme wake (reality). Na mwanamke hana ujasiri wa kuomba msamaha kwa mme (reality).

Kurudisha hali ya hewa, mwache kama wiki moja au mbili, then mwombe msamaha kwa jinsi ulivyoufikisha ujumbe. Halafu mwache tena. Baada ikipita kama miezi miwili au mitatu mwambie kama hataki tena kuitumia hiyo gari unaigawa kwa mtu mwingine (hasa ndugu wa upande wako) au unafikiria kuiuza.

Kwa mwanamke subira yavuta heri. Mwache kwa muda. Ila onesha concern kuwa kitendo chake hicho hakikufurahishi! Atajirudi tu!
 
Kuna vitu vingine siyo vya kuleta hapa JF. kuna vitu ambavyo vipo ndani ya control ya mwanaume ndani ya nyumba. Hiki ni kimojawapo.
Ok..sikulaumu lakini, labda ulitaka kutuonyesha idadi ya magari uliyonayo. Tumekupata mkuu

Rejao, hoja yangu si idadi ya magari. Gari si fahari kama zamani ni kitendea kazi tu. Hoja ni hiyo tabia ya kuzira anapokosolewa. Umekuwa too subjective. Nashukuru nimekuelewa.
 

Nimeipenda hii. Mizizi ya tabia kama hii wakati mwingine ni malezi na kuwa too defensive. Nadhani nahitaji ku concentrate ktk vitu muhimu na kumwacha azire mpaka achoke. Mie nasonga mbele na mapambano ya maisha.
 
inaonyesha mkeo ana hasira sana
kwann mpaka atume sms kwani nyumbani harudi (kaonyesha dharau kwako)
ss we usimuulize kaa kimya mpaka hasira zitakapoisha.
 

wakati mwingine mtu anakua mzembe mzembe inabidi kumtreat kama toto dogo...mtu akiwa straight na makini na mambo yake utaanzaje kumcontrol?
 
Huyo ili kumridhisha afurahi fungua taa zako site mirror ukiweza na kioo cha dirishan viweke kwenye buti then mwambie mke wang na mie leo wameniibia utaona atakavofunguka kwa furah si nilikwambia we unasema mie mzembe.
 

Tayari vijana wa Kariakoo wanakumegea huyo mke we fatilia utagundua tu au unipe kazi hiyo mm nikuchunguzie kiintelejinsia.
Na jamaa zangu k.koo wengi kwenye maduka ya nguo na simu wabaya sana kwa wake za watu wanao fanyabiashara madukani.
Mzazi hapo lazima unakandamiziwa, funga biashara mwambie akae home akipika na kupakua.
 
mkuu wazazi wenu wote wana magari?hilo gari litengeneze vizuri uwapelekee kijijini mzee naye aienjoy.hawa viumbe wanaumiza kichwa sana.usitake kupigishana naye kelele.Muache aongee mwenyewe atachoka coz ukijifanya kumjibu mwisho wake utampiga makofi.chunguza mienendo yake.mke akianza dharau kua nae makini.wajue marafiki zake na vijiwe vyake.hawa viumbe hawapendi kukosolewa ndo maana anasema unamsimanga.pole sana.mia
 
Kuna wanaume wanajua kuwasimanga wake zao, hadi huruma

Yeah wakati mwingine unaweza kuwa ulisema ukapitiliza inatutokea; nami ni shahidi bahati nzuri kuna muda wa kujirudi maisha yanaenda.....kupishana kupo ndani ya nyumba usichukulie kiviiile!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…