Mke kuwafukuza ndugu wa mme ni halali

Wajameni tubadilike. maisha ya sasa siyo ya miaka ya 40 yale waliokuwa wanaishi mababu zetu vijijini. Maisha ya sasa katika nyumba ni mume mke na watoto basi; kuonana au kukutana na ndugu iwe kwa sababu maalum kwa kutembeleana kwa muda mfupi tu; Sio watu kuhamia bila sababu. Migogro mingi ya nyumba zetu inaletwa na ndugu. Mlioana wawili mle raha maisha, leo mnajipa kiwingu kwa kuleta ndugu ndani ya nyumba. Kama ni misaada wasaidiwe wakiwa hukohuko. Ikitokea ni ishu za maradhi hapo sawa, aje atibiwe akipata nafuu safari akaendelee kutumia dawa akiwa kwake. Mtawapa ubaya wake zenu bure wajameni. Watu wanaoongoza kuharibu nyumba ni kina mama wa mabwana maana wanaamini hakuna mke aliewahi kuwa bora kuliko wao. pili mawifi. So if unataka kuishi maisha mazuri na mkeo rekebisha utaratibu kuhusu ndugu. Another thing, no matter what you will do, bado utapata lawama tu
 
mimi nilishafukuza m1, ni bint na alikua mwanafunzi wa kidato cha 2, tulimchukua kijijini kwa mama yk mkubwa kuja kumsaidia apate elimu nzuri mjini, alipozoea mazingira ya mjini akaanza kunidharau kwa kigezo cha kwamba pale ni kwa mjomba wake (Mume wangu) hivyo atafanya atakalo na mtu asimbabaishe, nilimvumilia sana huku tukiendelea kumuonya, siku niliyoamua kumrudisha kwao ni siku aliyopika chakula (wali) kilo mbili akala kidogo kilichobaki chote akatupia kuku,kutoka kazini nikaelezwa na house girl kumuuliza akasema ANAYELETA CHAKULA NI MJOMBA WAKE yn mume wangu. Sikuwa na la zaid nilimwambia afungashe virago vyake asubuhi nikagonga gia kumrudisha kijijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…