Mke/Mme ulimpata katika mazingira yapi?

Mke/Mme ulimpata katika mazingira yapi?

Michael Edson

Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
36
Reaction score
63
Wakuu ndani ya mjengo nawasalimu.

Niwasilishe kwa ukumbusho kidogo hususani kwa wale tayari walioko kwenye Ndoa. Mkeo au mmeo uliyenae mpaka Sasa ulimpata katika mazingara yapi? Jamii yetu ya kiafrika tumekuwa watu wa kuoa au kuolewa kwa kufata kanuni na taratibu na kuzingatia zaidi itikadi za kiimani.

Mbali na hayo hivi Sasa kizazi cha kileo wengiwao imekuwa si kama ilivyokuwa huko nyuma nazungumzia bibi/babu zetu au wazazi wetu hasa kwa sisi kidgo tulio zaliwa miaka ya 80, ambao swala zima la kuoa au kuolewa haikuwa kama ilivyo Sasa.

Mimi sio mwandishi mzuri, nisimalize uhondo. Huyo bibi au bwana uliye nae ulimpataje? Nawasilisha kwenu.

1618743253975.png
 
Kanisani

NB

Sikua muimba kwayA wala mtoa huduma yoyote kanisani....nae hivyo hivyo......

Kwa niliyopitia nilimuomba Mungu wa kufanana nae nikutane nae katika nyumba yake .........

Nikasahau nakusahau hata nilipitia nini na niliomba nini...

Mwaka mmoja baadae paaaap huyu hapa!!!!!!!!!

Tunazeeka tu sa hii...

Oooophs leo nimefunguka daaah!!!!!!!!

Mchana mwema!!!
 
Huyo ni mkeUlikwisha muamdaa toka utotoni huko ikawa kumbukizi na kutimiza wajfu.
wala sikumuandaa tulipotezana 18 yrs, hatukuwa na yoyote mahusiano utotoni ,nili like kapicha Fb ,nikaulizwa inbox are you obama wa bongo nikamjibu yes ni mimi.. akaniomba simu no anisalimie nikampa! kwenye stori akaniuliza unafanya kazi wapi nikamtajia,Kumbe kila mara anakuja ofisini kwetu ila kitengo tofauti... mara kaanza kupita na ofisini kwangu kunisalimu kama mdogo wangu anajitambulisha ili ahudumiwe fasta...baada ya miaka 2 kasoro nikasema haiwezekani lazima nimtafune hakuna cha ukaka hapa japo nilikuwa kwenye uhusiano mwingine wenye changamoto ! Duh kutest tu imooo,yaaani sikupata pingamizi lolote , miezi najishangaa tu nipo madhabahuni ,nauza uhuru wangu kwa huyu binti 🥰🥰🥰 ishu ilikuwa tu ofisini wanashangaa uonao mdogo wako??......Haya maisha bhana
 
Back
Top Bottom