Mke/Mme wa Mjomba/Shangazi

Mke/Mme wa Mjomba/Shangazi

IshaLubuva

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2008
Posts
250
Reaction score
11
Waswahili hebu nijuzeni kwenye hili; Mke/Mme wa Mjomba/Shangazi wangu/yangu ni mwite nani?. Je ni sahihi kumwita Shaangazi/Mjomba?.

Karibuni nguli wa kiswahili kwa mjadala.
 
eti anaitwa mkaza mjomba, huyo ni mme wa shangazi yako hahahahaha
 
Nimeangalia kwenye Kamusi ya TUKI halimo hilo. Kwani wewe hauna Shangazi Chimunguru?

najua kwenye kamusi halipo ila nimeuliza watu tofauti wanataja jina hilo hilo. shangazi nnao wengi tu!
 
Baba shangazi=mume wa shangazi.

Mkaza mjomba=mke wa mjomba.

Source: eneo nililokulia mimi (mtaani kwetu aka uswazi).
 
....... Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.
 
....... Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.
.

Haya ni matumizi ya kimazoea (kama ambavyo tumezoea kuwaita watoto wa Dada zetu Mjomba na nyie kina Pretty mnawaita watoto wa Kaka zenu Shangazi wakati wanatakiwa kuitwa Wapwa/Mpwa) ambayo hata mimi nayafahamu. Kwenye Fasili (definition) Mjomba ni ndugu wa kiume wa Mama mzazi wa ..... na Shangazi ni Dada wa Baba Mzazi wa ....
 
kweli kiswahili hakijajitosheleza au kimekufa
nimeamini sijui kiswahili kabisa
 
....... Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.
Vile vile tunaweza kutumia Mkwe kwa mke wa Mjomba na Baba kwa mume wa Shangazi. Siamini kuwa Kiswahili hakijitoshelezi kama ilivyodaiwa hapa. Naili waomba wana JF wakumbuke kuwa Kiswahili si kimoja, kama ilivyo kwa lugha nyingi kuu. Kiswahili cha Tanzania sio Kiswahili cha Kongo wala Rwanda au Somalia, kama ilivyo kwa Kiingereza cha London sio sawa na Kiingereza cha Wales, Ireland au Scotland. Inawezekana hata Pwani au Bara watu wa maeneo mbali mbali wakawa wanatafautiana maana ya baadhi ya maneno. Isifikirie kwa mfano, Wazanzibari wote wanazungumza Kiswahili kimoja. Inapotokea matatizo kama haya ni bora kukimbilia kwenye Kiswahili Sanifu na bora zaidi Kamusi ya Maana na Matumizi.
 
....... Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.
Kwangu mimi Mke wa Mjomba ninamwita Mama mjombaau Mkwe ,na mume Wa Shangazi nitamwita Mjomba
 
Back
Top Bottom