IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 11
eti anaitwa mkaza mjomba, huyo ni mme wa shangazi yako hahahahaha
Nimeangalia kwenye Kamusi ya TUKI halimo hilo. Kwani wewe hauna Shangazi Chimunguru?
........ Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.
Vile vile tunaweza kutumia Mkwe kwa mke wa Mjomba na Baba kwa mume wa Shangazi. Siamini kuwa Kiswahili hakijitoshelezi kama ilivyodaiwa hapa. Naili waomba wana JF wakumbuke kuwa Kiswahili si kimoja, kama ilivyo kwa lugha nyingi kuu. Kiswahili cha Tanzania sio Kiswahili cha Kongo wala Rwanda au Somalia, kama ilivyo kwa Kiingereza cha London sio sawa na Kiingereza cha Wales, Ireland au Scotland. Inawezekana hata Pwani au Bara watu wa maeneo mbali mbali wakawa wanatafautiana maana ya baadhi ya maneno. Isifikirie kwa mfano, Wazanzibari wote wanazungumza Kiswahili kimoja. Inapotokea matatizo kama haya ni bora kukimbilia kwenye Kiswahili Sanifu na bora zaidi Kamusi ya Maana na Matumizi........ Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.
Kwangu mimi Mke wa Mjomba ninamwita Mama mjombaau Mkwe ,na mume Wa Shangazi nitamwita Mjomba....... Mke wa mjomba anaitwa shangazi........na mume wa shangazi anaitwa mjomba. Makabila mengi tu yanaita hivi, hata kwetu tunatumia majina haya.