Mke Msomi + Mume Msomi = Ndoa nzuri yenye mafanikio?

Safi sana hili tumeliona sana hata fweza nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa mwanamke akiwa na kipato kikubwa dah hashikiki nyumbani

hapo kny pesa ndo usiseme mwanaume anaweza kufanywa kitu mbaya
 
hapo kny pesa ndo usiseme mwanaume anaweza kufanywa kitu mbaya

Hahahaha mwanaume anakuwa kama mbwa koko anageuzwa zuzu watoto wa mujini wanasema bushoke lol

Na usiombee mama anunue usafiri wa nguvu kama V 8 zile za JK au awe na hummer mashosti mtakoma kulinga
 

Ndoa ni maelewano, na mnapokutana regardless of your background kinachowakutanisha ni penzi, baada ya muda ndio mnaanza kujuana tabia,ndugu na kisomo

Kwa upande wangu mimi na mume wangu kielimu tuko sawa ila tunafanya kazi tofauti, mwaka huu Mungu akipenda tutatimiza miaka 7 bila kokoro wala kelele I thank God daily for meeting and calling this man my husband,

Mambo tunayobishania hapa home mara nyingi sana ni future plans kama kubadili kazi,ujasiriamali etc maana kila mtu ana maono yake but we compromise,

Hatujawahi kuhitlafiana kuhusu elimu kwa watoto or matumizi ya pesa zetu za mshahara, kila mmoja anakatwa kiasi sawa kwa mwezi kuingia ktk account za watoto
 
Hahahaha mwanaume anakuwa kama mbwa koko anageuzwa zuzu watoto wa mujini wanasema bushoke lol

Na usiombee mama anunue usafiri wa nguvu kama V 8 zile za JK au awe na hummer mashosti mtakoma kulinga

hahahaha!hapo sipati picha ni Fidel anafanyiwa hivyo,,muda wote maskini unakuwa mdogo kama piriton,,unakosa konfidensi ya kiume kabisa yani unakuwa wewe ndo umeolewa,,dah!God have mercy
 
hahahaha!hapo sipati picha ni Fidel anafanyiwa hivyo,,muda wote maskini inakuwa mdogo kama piriton,,unakosa konfidensi ya kiume kabisa yani unakuwa wewe ndo umeolewa,,dah!God have mercy

Asikwambie mtu Pesa ina nguvu bana angalia mitaani kijana mdogo mwenye pesa anavyo nyenyekewa wazee wanampa shikamoo sasa sembuse pesa kaikamata mwanamke kwenye ndoa hiyo si kutakuwa na nidhamu za woga unashangaa nampa wife shikamoo asubuhi kisa anakisu kirefu
 

hahaha!ukweli ni kwamba mwanamke hata akiwa na pesa isizidi ya mwanaume,,ingawa zaidi ni kumuomba Mungu kupata mwenza mwema.:A S-alert1:
 
hahaha!ukweli ni kwamba mwanamke hata akiwa na pesa isizidi ya mwanaume,,ingawa zaidi ni kumuomba Mungu kupata mwenza mwema.:A S-alert1:

Waswahili wanasema pesa ni sabuni ya roho ukiwa nazo mmh sijui kama utamkumbuka Mungu kwa dhati zaidi zaidi itakuwa unafiki tu
 
Waswahili wanasema pesa ni sabuni ya roho ukiwa nazo mmh sijui kama utamkumbuka Mungu kwa dhati zaidi zaidi itakuwa unafiki tu

Dah!hapo sasa itabidi uje huku nikuombee upako ili uanze kuomba sasa hivi usije kufanywa bushoke bdae
 
hahaha!ukweli ni kwamba mwanamke hata akiwa na pesa isizidi ya mwanaume,,ingawa zaidi ni kumuomba Mungu kupata mwenza mwema.:A S-alert1:
I beg to differ, we shouldn't submit to have lesser pay because we are married and are scared to bruise our men's ego,
We can only say, for higher earners respect should be both ways, but leo nikipata promotion yenye more money than hubby niikatae cause he's head ?
He can still be the head even when I earn more, kikubwa ni upendo, maelewano na ushirikiano, to me money doesn't matter @ all
Mhandisi
 
Kwa uzoefu wangu wa wanamume,hakuna mwanamume mdogo hata awe hajasoma atataka kuwa juu, inaboa sana...Ni bora kuwa na ndoa ya mwanaume na mwanamke wote mmesoma kuliko mi mwanamke nimesoma mume wangu hajasoma.......kwanza wanakuwa na kuona wanadharauliwa(inferiority) na hawajiamini na katika kitu kibaya kupata ni mwanaume asiyejimini,ina ku turn off kila kitu na kila kitu anabisha ili mradi uanamme wake uonekane,huh........kuna wenye bahati ya kupata wanaume waelewa wasiosoma ukimpata well and good.
 
ukweli nnikwamba lazima tujaribu kuchagua wenza tunaoendana kidogo kwenye elimu zetu nimeona ndo zenye wake wasiosoma na mume kasoma ni tatizo mmoja nilishuhudia alikuwa hataki kutoka na mkewe anapokutana na watu wa ofisini kwake ,mwingine mjadala ukianzishwa sikiliza point za baba na mama mwisho wa kikao lazima wagombane mume anaona kama mke hamna analojua anaongea ongea tu

na mke anapokuwa msomi zaidi ni tatizo mara nyingi tunajijua sisi tulivo hilo halipingikiki mwanaume itabidi akubali na kupika,kuosha mtoto,saa zingine anaweza hata kudeki ili ndoa iendelee kuwepo
 
but leo nikipata promotion yenye more money than hubby niikatae cause he's head ?
Mhandisi

Ndugu Mhandisi
Kama unajua binadamu tunabadilika kulingana na mda, mahali n.k basi elewa leo hii wewe ukiwa bilionea kuliko mmeo lazima ndoa yako iingie mushkeli piga ua galagaza, wewe mwenyewe utabadilika kwa mmeo na hii italeta mfarakano zaidi na zaidi na jamaa kujiona mtumwa kwako bilione
 
Dah!hapo sasa itabidi uje huku nikuombee upako ili uanze kuomba sasa hivi usije kufanywa bushoke bdae

Hapo sawa sawa mama akiwa bilionea pesa zote anikabidhi mm niwe nakontrolo kila kitu Mungu nijalie bahati hii
 
awe mwishooooooooo kabisa degree ya biashara or diploma
 
Baba Phd holder, mama na MBA....Yaani kitanda kimoja zinalala digrii tano...Dah!
 
Baba Phd holder, mama na MBA....Yaani kitanda kimoja zinalala digrii tano...Dah!

Mkuu you made a day kwangu....
Kuna wengine maprofweza wanashea kitanda...
 
Tumeongelea sana elimu, pia kuna vyeo au madaraka hata kama wote ni wasomi. Mke akiwa na madaraka makubwa kumpita mume inaweza kuleta shida fulani aidha kwa mke kujiona yuko juu au mume akawa na complex inferiority!!
 
Can we look @ some successful women out there who make more money and if their marriage ziko strong ? Nahisi umuhimu ni heshima jamani,
mbona mimi niligraduate na kuanza na kazi nzuri kabla ya mume ?
Mume amegraduate nyuma yangu (maana aliunganisha na masters ) na sasa ana kazi nzuri zaidi yangu lakini sikuwahi kumdharau kwa kuwa na mshahara mkubwa mwanzoni...

Kuna mawaziri, wabunge, wakurugenzi wengi tu wenye stable marriages na more money lakini wana ndoa imara

Sasa na mimi nawania kazi fulani na niko kwenye mchakato wa usaili , na nikiipata nitakuwa posted nje ya nchi...niiachie tuu hivihivi jamani ?? ( Worried!! ) Wkt hubby is so supportive !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…