Mke/mume safi mume/mke kicheche kuepuka hii. . Kagua unachofikiri

Mke/mume safi mume/mke kicheche kuepuka hii. . Kagua unachofikiri

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Nafikiri mmeshawahi kusikia watu wakisema "aah ukikuta mume ametulia mke lazima hajatulia"(and vise vesa) au kauli kama "kwenye miti hakuna wajenzi".Yote haya yanatokana na watu kupata "wasiyotarajia"!Lakini mimi nasema walistahili.Nasema hayo nikiwa ninajua kosa walilofanya.Unajua vijana wengi linapokuja suala la wenzi wa maisha au uhusiano huwa tunajawa na hofu,hofu hizi hutokana na namna ambavyo watu hawajatulia kimahusiano siku hizi,hupelekea kuanza kujiuliza,"sijui nitaangukia kwa nani Mungu wangu".Mawazo haya hupelekea vijana kufanya kosa kubwa sana,kosa hilo ni kutumia muda mwingi kama sio wote kuwafikiria wenye tabia mbaya.Jambo tusilolijua ni kwamba wanadamu tuna mawazo ya kawaida na yale ya kina.Mawazo ya kawaida sote tunayajua.Mawazo ya kina kazi yake ni kuvuta kile kinachopelekwa huko baada ya kukaa kwenye mawazo ya kawaida kwa kipindi kirefu kidogo.Hivyo basi tunapotumia muda mrefu kuwaza kuhusu jambo fulani jambo hilo hupelekwa kwenye mawazo ya kina kwaajili ya utekelezaji.Unapowaza jambo fulani muda mrefu unayaambia mawazo ya kawaida kuwa unaliihitaji jambo hilo.Hii ni kanuni ya maumbile,uwe unajua au hujui.So kwenye mahusiano unapofikiria sana kuhusu mtu wa tabia fulani jua unamvuta kwako ndo utakua karibu nae tu.Na bahati mbaya jamii imetufundisha kuwaza mabaya.Umewahi kujiuliza ni kwanini mtu mwenye kisirani anakutana na wenye kisirani kirahisi?Watu wenye tabia njema huwawaza sana wenye tabia mbaya kwa kuhofia kuwa nao kumbe ndo wanawavuta!Kama unataka mazuri waza mazuri!
 
Hi Eiyer, niko airport mwanza napita lkn!
Nice thread though.
 
Hi Eiyer, niko airport mwanza napita lkn!
Nice thread though.

Ha,ha,ha,ungeniDIPU nije nikulete hata maji ya kunywa,niko nje hapa. . . . . . Thanx for kwa kuikubali siredi!
 
Ha,ha,ha,ungeniDIPU nije nikulete hata maji ya kunywa,niko nje hapa. . . . . . Thanx for kwa kuikubali siredi!

I know, ila ungeniletea Sato wa kuchomwa kwenye aluminum foil ningependa zaidi!
 
I know, ila ungeniletea Sato wa kuchomwa kwenye aluminum foil ningependa zaidi!

Nini vile?Alumuniom fuoilu ndo nini tena,ni jiko la mkaa au kuni?
 
Back
Top Bottom