Mke, mume wafa kwenye ajali iliyoua sita Kiteto

900 Itapendeza zaidi

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2017
Posts
7,704
Reaction score
9,186
Ajali hiyo imetokea eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya gari la wagonjwa kugongana uso kwa uso na gari dogo.

Watumishi sita wa Serikali, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wakiwamo mke na mume, wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya kupata ajali ya gari eneo la Pori wilayani humo.

Watumishi hao kati yao watano wanatoka Idara ya Afya na mmoja Idara ya Elimu, kwa pamoja wamepoteza maisha baada ya gari lao walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na gari lingine aina ya Prado.

Tukio hilo limetokea jioni ya jana Jumatatu Novemba 07, 2022 eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto na kupelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga, akiwa hospitali ya Kiteto amethibitika kutokea ajali hiyo.

Alisema ajali hiyo imehusisha gari la wagongwa la Kituo cha Afya Sunya lililokuwa limepeleka mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa ajili ya matibabu na wakati likirudi likiwa limebeba watumishi kurejea eneo la kazi Sunya liligongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Prado likitokea barabara ya Kilindi Tanga kwenda Kiteto.

"Ajali hii imehusisha gari letu la afya ‘ambulance’, Kituo cha Afya Sunya ambalo limegongana uso kwa na gari lingine dogo aina ya Prado na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi watano wamepelekwa hospitali ya Dodoma, wangine wawili wanaendelea na matibabu hospitali ya Wilaya ya Kiteto" alisema Batenga.
Taarifa zinasema kati ya waliofariki ni mume na mke ambao wameacha mtoto wa miezi nane.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kiteto, Pascal Mbota akizungumza na Mwananchi Digital alisema amepokea miili ya watu wawili waliopoteza maisha na majeruhi kumi na moja.

Kati ya majeruhi hao wanne wamefariki katika harakati za kuokoa maisha yao, watano wamesafirishwa kwenda Hospitali ya Dodoma kwa matibabu na wawili wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya Kiteto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi, alithibitisha ajali hiyo akisema atatoa taarifa kamili baadaye.
ajali-pic.jpg
 
Ni mhimu kujiandaa kwamba kifo kipo, unyakuo ukicheleweshwa kifo kitakujia ghafula! Na baada ya kifo hamna Toba yoyote inayoweza kufanyika kwa huyo aliyekufa!! Sio kwamba wewe na mm tulio hai leo kuwa tumetenda mema Sana hapana, Mungu amekuacha hata leo uweze kutubia uovu wako, umekuwa mzinzi, mwasherati, mlevi, mgomvi, mwenye hasira, mwizi wa pesa za walipa Kodi, umejilimbikizia Mali ya umma, Wala huwazi kwamba kifo kipo, una kiburi cha maisha, una kiburi cha elimu yako! Hutaki kumjua Mungu na nguvu zake, hutaki hata kumuulizia huyu Yesu ni nani!! Ole wako! Usikifikiri Mungu ni mjinga kama wewe, wanadamu kutokana na elimu zetu, Mali zetu, vyeo vyetu na umaarufu wetu tunakuwa na kiburi, na jeuri, anaona kuwa ataishi milele duniani ole wako! Mungu sio mjinga kama wewe, amekuacha tu ili angalau ukumbuke kutubu ndo maana upo hai mpaka leo, usidhani Mungu haoni uovu wako! Dhamira yako inakushuhudia maovu lakini umekuwa mkaidi na mgumu kutubia uovu wako ole wako wewe!!! Siku inakuja, kiburi Cha fedha yako, umaarufu wako, elimu yako, utaona ni takataka na bahati mbaya hautakuwa na nafasi nyingine ya kutubu!

Warumi 2:5
Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu,

Warumi 2:6
atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;

Ufunuo wa Yohana 14:13
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Mathayo 24:42
Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu.

Mathayo 24:43
Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa.

Mathayo 24:44
Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.
 
Ni mhimu kujiandaa kwamba kifo kipo, unyakuo ukicheleweshwa kifo kitakujia ghafula! Na baada ya kifo hamna Toba yoyote inayoweza kufanyika kwa huyo aliyekufa!! Sio kwamba wewe na mm tulio hai leo kuwa tumetenda mema Sana hapana, Mungu amekuacha hata leo uweze kutubia uovu wako, umekuwa mzinzi, mwasherati, mlevi, mgomvi, mwenye hasira, mwizi wa pesa za walipa Kodi, unajilimbikizia Mali tu, wala huwazi kwamba ipo

Amen!
Mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie.
 
Nani kakudanganya ulevi ni dhambi?

Huwa najiuliza; hivi hizi ajali za barabarani tunazopata hapa Tanzania, na wenzetu nao wanapata kama sisi? Kama hawapati kama sisi, sisi ni watu wa aina gani ambao kila wakati ajali ziwe zetu?

Hebu tuangalie wenzetu wa nchi kama za Ulaya au Marekani, huwezi kusikia mambo kama haya yakitokea mara kwa mara. Ikitokea, basi ni bahati mbaya sana, na hautasikia tena mpaka baada muda mrefu sana. Hata hapo Kenya tu na Uganda, huwezi kusikia habari za ajali za kipumbavu kama hizi.

Sasa hebu tujiulize, hivi sisi ni watu wa aina gani hata tusijifunze kutokana na matukio (ajali) ya nyuma? Je, ni wagumu sana kuelewa? Tuna vichwa vya aina gani hata tushindwe kuzingatia usalama barabarani?

Kuna watu wanasema ni bahati mbaya, na wengine wanasema ni kazi ya Mungu; hivi kweli mtu afanye upumbavu wake halafu tuseme kazi ya Mungu?! Tunaweza kuona ni mambo ya kawaida, lakini wenzetu huenda wanatushangaa sana kutokana na mienendo yetu.

Bahati mbaya ikitokea, tujifunze jambo, sio tunabaki vilevile. Tunakuwa kama kuku, ambaye ukimpiga baada kula chakula ulichomkataza, anakimbia lakini baada ya muda mfupi anasahau maumivu aliyopata, anarudi kufanya kosa lilelile. Jamani tuache upumbavu na ujinga?!
 
Ajali hiyo imetokea eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya gari la wagonjwa kugongana uso kwa uso na gari dogo.

Watumishi sita wa Serikali, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wakiwamo mke na mume, wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya kupata ajali ya gari eneo la Pori wilayani humo.

Watumishi hao kati yao watano wanatoka Idara ya Afya na mmoja Idara ya Elimu, kwa pamoja wamepoteza maisha baada ya gari lao walilokuwa wamepanda kugongana uso kwa uso na gari lingine aina ya Prado.

Tukio hilo limetokea jioni ya jana Jumatatu Novemba 07, 2022 eneo la Pori namba moja Kata ya Partimbo wilayani Kiteto na kupelekwa hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga, akiwa hospitali ya Kiteto amethibitika kutokea ajali hiyo.

Alisema ajali hiyo imehusisha gari la wagongwa la Kituo cha Afya Sunya lililokuwa limepeleka mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa ajili ya matibabu na wakati likirudi likiwa limebeba watumishi kurejea eneo la kazi Sunya liligongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Prado likitokea barabara ya Kilindi Tanga kwenda Kiteto.

"Ajali hii imehusisha gari letu la afya ‘ambulance’, Kituo cha Afya Sunya ambalo limegongana uso kwa na gari lingine dogo aina ya Prado na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi watano wamepelekwa hospitali ya Dodoma, wangine wawili wanaendelea na matibabu hospitali ya Wilaya ya Kiteto" alisema Batenga.
Taarifa zinasema kati ya waliofariki ni mume na mke ambao wameacha mtoto wa miezi nane.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kiteto, Pascal Mbota akizungumza na Mwananchi Digital alisema amepokea miili ya watu wawili waliopoteza maisha na majeruhi kumi na moja.

Kati ya majeruhi hao wanne wamefariki katika harakati za kuokoa maisha yao, watano wamesafirishwa kwenda Hospitali ya Dodoma kwa matibabu na wawili wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya Kiteto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara RPC George Katabazi, alithibitisha ajali hiyo akisema atatoa taarifa kamili baadaye.
View attachment 2410062
20221108_112541.jpg
 
Back
Top Bottom