Mke uliyenae ungekuwa sasa unamchumbia ungemuoa??

Mke uliyenae ungekuwa sasa unamchumbia ungemuoa??

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
MKE U
Kati ya mambo muhimu ambayo binadamu yeyote huota siku moja akutane nayo ni siku ya harusi kama kaka Gilbert Mongi na dada Bertha Mlay wakati ya sherehe ya harusi yao Istana jijini Dar es Salaam tarehe 26/07/2008
(Picha kwa hisani ya fomafoma blog)
Kuna mahali wanandoa waliulizwa swali hili:
Je, mke uliyenaye au mume uliyenaye sasa kama ingetokea sasa hivi iwe ni ule wakati unachumbiana naye kuwa mke au mume ungemchagua kuoana naye?

Zaidi ya asilimia 70 walisema wasingekuwa tayari kuoana nao kwani wamegundua kuna tofauti kubwa sana ya mtu aliyenaye sasa na yule alikuwa kabla ya kuoana.

Je, wewe ungeliulizwa swali hili leo ungekuwa na jibu gani?
Ukweli jibu unalo wewe ndani ya moyo wako na ni siri yako.

Ukitaka kujua ndoa yako ina joto kiasi gani unaweza kujibu maswali yafuatayo kwa usahihi na uaminifu kabisa kwa kuchagua jibu sahihi kwako.

1. Tunaweza kumaliza mgogoro au tofauti ya mgongano wa kimawazo chini ya dakika 15.
A. Hata siku moja.
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

2. Huwa tuna tabia ya kumaliza matatizo yetu kabla ya kulala
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

3. Huwa nawaza kuhusu talaka
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

4. Namkumbatia na kumpa busu mpenzi wangu kwa mahaba
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

5. Mapenzi katika ndoa yetu yanaridhisha sana
A. Hata siku moja
B. Mara chache sana
C. Mara kwa mara
D. Mara zote

Hadi hapo naamini umepata picha kamili ya wapi unaelekea na mpenzi wako.

Je, yafuatayo nayo ni wimbo wa kila siku katika ndoa yako?
Kama ni kweli basi unahitaji msaada haraka iwezekanavyo.

Mawasiliano ovyo
Hakuna tendo la ndoa na kama lipo basi ni bora wajibu hakuna ladha halisi
Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
Hakuna mahaba
Hakuna kutiana moyo wala kupeana asante
Migogoro isiyoisha
Kuumizana kihisia
Kukosa uaminifu kati ya mwanandoa
Migogoro ya matumizi ya fedha
Tabia ya kukefyakefya


LIE NAE UNGEKUWA SASA UNACHUMBIA UNGEMWOA??
 
Ndo maana kuna huu usemi.."mwakimbilia ingia... sie twajutia kuwemo".. nahisi msemo huu una apply
 
come back here wewe......umeulizwa...utamwuwowa au usingemwuwowa.....simple........

wenzako waliletewa na shangazi wanasubiri kumuuliza shangazi ajibu watuletee wape muda mwaya wasije.....mmmmh lakini leo man u wamtutenda we acha tu
 
come back here wewe......umeulizwa...utamwuwowa au usingemwuwowa.....simple........
Mmmh wewe lazima tu utakuwa ni mtani wangu kutoka kule Ziwa Magharibi....Utamuwowa au utamusewla...!.
 
wenzako waliletewa na shangazi wanasubiri kumuuliza shangazi ajibu watuletee wape muda mwaya wasije.....mmmmh lakini leo man u wamtutenda we acha tu

hicho kinaitwa kipigo cha Eid El Fitr.........mtajibeba.....(japo hata mimi ni mshabiki wa Arsenal)
 
Mmhhh mao leka tupu inu ngafila mpaka ngaamba basi
 
my... my...my.... Mbona kaka zetu hamjibu??

Hamhitaji kujibu kwa urefu ... naona Pd kaamua iwe

multiple choice....lol.. Kazi kwenu... Power to you....
 
Mara mia ungeniuliza swali hili ningekujibu, ndio. Sina shaka ningekubali kuolewa na niliyenaye leo!
 
Hii maalum kwa walioko kwenye hili gurudumu,kwa tulio nje tunakua kama watazamaji!
 
Kumbe ni Special for married people.....jameni napita tu narudi kwenye kitandani changu
 
wenzako waliletewa na shangazi wanasubiri kumuuliza shangazi ajibu watuletee wape muda mwaya wasije.....mmmmh lakini leo man u wamtutenda we acha tu
Hehehe!!! Pole sana Pdidy uchungu wa magoli aujuaye ni Wenger lol!!!
 
dah ningemuwowa lakini co haraka kama nlivyowowa bana kuna vijitabia ngumu au vinachukua muda mrefu kumech
 
Naona wanaume wamegoma kujibu; wamepata kigugumizi. Mimi mume niliyenaye pamoja na mapungufu ya hapa na pale ambayo nimekuja yagundua baada ya kuishi several years; nikiangalia nyuma na kukagua wale niliokuwa nao kabla ya kuolewa, he is still the choice now and forever. Sijawahi ku regret ile ya bora ningeolewa na fulani. Nope. Wote ambao wangeweza kuwa kwenye nafasi yake maisha yao na wake zao wala hayani impress.
 
Back
Top Bottom