Kizza Besigye na Yoweri Museveni walikuwa marafiki walioshibana wakati wa Vita ya Msituni Uganda kumuondoa Milton Obote miaka ya 1980, na Dkt. Besigye aliwahi kuwa daktari binafsi wa Museveni na wanajeshi wengine waliokuwa msituni pamoja na Museveni
Rais Museveni na Winnie Byanyima walikuwa wachumba kati ya 1981 na 1986, Bi Byanyima alikuwa pamoja na Museveni alipoingia Kampala akiwa mkuu wa jeshi la waasi mwaka 1986. Lakini Museveni hakuwa tayari kumuacha mkewe, Janet, na Bi Byanyima akafukuzwa. Hatimaye aliolewa na Dkt. Besigye 1998.
Inadaiwa kitendo kile kilimuuma sana Rais Museveni, kwanza akataifisha ranchi ya babake Winnie Byanyima, Mzee Boniface Byanyima.
Pia matukio hayo ya ngono na usaliti yalijenga uadui mkubwa kati ya miamba hiyo ya siasa nchini Uganda.
Yoweri Museveni akisalimiana Amos Kaguta (Babake) muda mfupi baada ya vikosi vya NRA kuliteka jiji la Kampala 1986. Aliyevaa magwanda ya kijeshi kulia ni Winnie Byanyima (Aliyekuwa Mchumba wake)
Kanali Dkt. Kizza Besigye akiwa na Winnie Byanyima enzi za uchumba wao miaka ya 90
Rais Museveni na Winnie Byanyima walikuwa wachumba kati ya 1981 na 1986, Bi Byanyima alikuwa pamoja na Museveni alipoingia Kampala akiwa mkuu wa jeshi la waasi mwaka 1986. Lakini Museveni hakuwa tayari kumuacha mkewe, Janet, na Bi Byanyima akafukuzwa. Hatimaye aliolewa na Dkt. Besigye 1998.
Inadaiwa kitendo kile kilimuuma sana Rais Museveni, kwanza akataifisha ranchi ya babake Winnie Byanyima, Mzee Boniface Byanyima.
Pia matukio hayo ya ngono na usaliti yalijenga uadui mkubwa kati ya miamba hiyo ya siasa nchini Uganda.
Yoweri Museveni akisalimiana Amos Kaguta (Babake) muda mfupi baada ya vikosi vya NRA kuliteka jiji la Kampala 1986. Aliyevaa magwanda ya kijeshi kulia ni Winnie Byanyima (Aliyekuwa Mchumba wake)
Kanali Dkt. Kizza Besigye akiwa na Winnie Byanyima enzi za uchumba wao miaka ya 90
- Tunachokijua
- Kizza Besigye Kifefe alizaliwa Aprili 22, 1956 nchini Uganda. Ni daktari wa binadamu, mwanasiasa, na afisa wa zamani wa kijeshi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda .
Aliwahi kuwa Rais wa chama cha siasa cha Forum for Democratic Change (FDC) na alikuwa mgombea ambaye hakufanikiwa kushinda katika chaguzi za urais za 2001, 2006, 2011 na 2016, dhidi ya Rais wa sasa wa uganda, Yoweri Museveni aliyeanza kutawala tangu Januari 26, 1986.
Urafiki wake na Museveni unatajwa kuanza miaka ya mwaka 1979 baada ya Besigye kujiunga na harakati za Museveni ambapo mwaka 1982, urafiki ulikwenda mbali zaidi kwa Besigye kuwa daktari binafsi wa Museveni.
Mnamo mwaka 1998, alimuoa Winnie Byanyima, ambaye wakati huo alikuwa mbunge wa manispaa ya Mbarara kusini magharibi mwa Uganda.
Uhusiano wa Winnie na Museveni
Ugomvi wa Besigye na Museveni unatajwa kuwa na mzizi ulioanzia nje ya ulingo wa siasa.
Disemba 2005, Benon Herbert Oluka, mwandishi wa Jarida la The Observer alifanya mahojiano maalum na Boniface Byanyima, baba mzazi wa Winnie Byanyima na Mwenyekiti wa zamani The Democratic Party (DP) aliyethibitisha madai ya Rais Museveni kuwa na nia ya kumuoa binti yake.
Mzee Byanyima alisema kuwa Rais wa sasa wa Uganda, Yoweri Museveni alipendekeza mara 2 kumuoa Winnie lakini aitupilia mbali maombi hayo kwa sababu Museveni hakuwa mtu wa kuaminika.
Boniface Byanyima akiwa na binti yake Winnie Byanyima
Maelezo haya yanapatikana pia kwenye makala ya Mei 22, 2017 iliyochapishwa na Jarida hilo hilo la The Observer.
Mzee Byanyima alienda mbali zaidi kwa kubainisha kuwa kiongozi huyo wa muda mrefu wa Uganda (Museveni) alikuwa akiishi pamoja na Winnie Byanyima huku tayari akiwa na Mke wake wa sasa Janet Kataaha Museveni.
Uchumba wao nje ya ndoa ulianza kutokana na mafanikio ya vita vya msituni vya Museveni vilivyoanzishwa kati ya 1981 na 1986 dhidi ya serikali ya Milton Obote, na baadae ile ya Tito Okello.
Byanyima katika mahojiano hayo alieleza jinsi alivyovunjika moyo baada ya binti yake mrembo Winnie alipojiunga na Museveni msituni huku yeye akitarajia kuwa atakwenda Ulaya baada ya kusomea shahada yake ya uhandisi katika Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza.
Byanyima alisema;
Museveni alipendekeza kumuoa mwanangu Winnie, jambo ambalo nililipinga na kumwambia binti yangu kuwa Museveni hakuwa mtu wa kuaminika. Nadhani ilikuwa mwaka 1987. Wakati huo alikuwa Amemuoa Janet (Kataaha). Nilijua hilo.
Kwanza alikuja baba yake Amos (Kaguta) kutoa posa. Nikasema hapana. Kisha Museveni akaja alipokuwa Rais. Nikasema siwezi kukubali. Nilisema ikiwa utamuoa.. akitaka, itakuwa ni jukumu lake. Sitaki hilo. Baadae walikaa pamoja kwa muda. Wakati watu wanakaa pamoja, hujui ni kwa muda gani (lakini) walikuwa wanakaa pamoja Entebbe.
Ndipo Winnie akagundua kuwa Museveni hakuwa mtu mzuri wa kukaa naye. Nadhani aligundua nilichomwambia kuhusu tabia ya Museveni, hivyo akamuacha Museveni na serikali yake.
Museveni alipokuwa Rais, baada ya mwezi mmoja au miwili, alianza kuja hapa. Alikuwa akija hapa kila wiki au kila mwezi kuniona. Kwanza, alikuja kuomba kuoa binti yangu, lakini nilikataa. Hakukasirika kwa sababu alijua nisingeruhusu. Aliichukulia kirahisi. Hilo halikumzuia kuja hapa mara kwa mara kusalimia. Aliendelea kuonekana rafiki.
Besigye alifahamu uwepo wa uhusiani kati ya Winnie na Museveni?
Hakuna taarifa nyingi zinazothibitisha suala hili.
Hata hivyo, Disemba 23, 2006 Jarida la IOL, moja ya kampuni zinazoongoza za maudhui ya majukwaa mbalimbali nchini Afrika Kusini, lilimnukuu Besigye akithibitisha kwamba alijua kuhusu uhusiano wa kimapenzi ambao Museveni aliwahi kuwa nao na mkewe, lakini akasema kuwa hiyo haikuwa sababu ya wawili hao kuwa na mikwaruzano mingi ya kisiasa. Alisema;
Ndio, walikuwa na uhusiano lakini sifikirii kama linahusika. Anachonifanyia Museveni anaweza kumfanyia mtu mwingine yeyote anayempinga.
Museveni anaweza kufanya matendo ya ukatili kwa mtu yeyote anayempinga. Yote yanahusiana na nguvu.
Hapo awali, gazeti huru la The Daily Monitor liliwahi pia kumnukuu mwanasiasa huyo akiambia kituo kimoja cha redio nchini Uganda kwamba hakuna shaka kuwa Winnie alikuwa na uhusiano na Rais Museveni lakini tofauti zake na Museveni zilikuwa za muda mrefu kabla hata ya kuwepo kwa uhusiano huo.
Pia, msemaji wa Besigye's Forum for Democratic Party, Wafula Oguttu katika nyakati fulani aliwahi pia kunukuliwa akisema Museveni bado anampenda Winnie na huenda asikate tamaa.
Museveni bado anampenda Winnie. Hajawahi kukata tamaa juu yake hadi leo. Nadhani Museveni ana mtazamo hasi dhidi ya Besigye kwa sababu ya Winnie.
Pia tunafikiri kwamba Museveni alimwona Besigye kama mtu ambaye hakumheshimu alipokwenda kinyume naye katika siasa.
Oguttu alidai Museveni alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi lakini ni Winnie pekee ambaye alikuwa na ujasiri wa kutosha kumwacha.
Habari za uhusiano wa Museveni na Winnie zinadokezwa pia na Jarida la The New York Times Juni 25, 2011 kwenye makala yao ya "In Uganda, a Bitter Rivalry Is Played Out on the National Stage"
Winnie Byanyima (64), Agosti 14, 2019 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa UNAIDS, nafasi anayohudumu hadi sasa.