Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mke wa Frank Mbise, kijana aliyetekwa zaidi ya siku 40, amemuangukia Rais Samia Suluhu Hassan, akiomba msaada wa kumrudisha mume wake nyumbani.
Akizungumza kwa uchungu, mwanamke huyo alisema kuwa amebaki katika hali ngumu akiwa na mtoto mdogo anayehitaji malezi na matunzo ya baba yake.
Ombi hilo limekuja baada ya Katibu Muenezi wa Baraza la Vijana Taifa, Twaha Mwaipaya, kumtembelea nyumbani kwake na kusikiliza kilio chake.
Soma pia: Mahakama yaamuru Polisi kuwatafuta viongozi wa BAVICHA (kina Deusdedith Soka) waliopotea
Mke wa Frank Mbise alieleza kuwa mume wake alikuwa tegemeo kubwa kwa familia yao, na kutekwa kwake kumeacha pengo kubwa, hasa kwa mtoto wao mdogo.
Kwa masikitiko makubwa, alisisitiza kuwa mume wake alikuwa mwema na alikuwa anatimiza majukumu yake kwa familia, hivyo kumkosa kwa muda mrefu kumeathiri maisha yao kwa kiasi kikubwa.
Amemuomba Rais Samia afanye kila juhudi kuhakikisha Frank Mbise anarudi salama uraiani ili familia yao iweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.